Oct 11, 2023 07:52 UTC
  • Rajoelina azindua kampeni kuelekea uchaguzi wa Rais Madagascar

Andre Rajoelina Rais wa Madagascar aliyemaliza muhula wake wa uongozi amezindua kampeni zake kuelekea uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika mwezi ujao nchini humo.

Katika kampeni hizo za uchaguzi wa Rais wa Madagascar, Rajoelina amewaahidi maelfu ya wafuasi wake, kile alichokitaja kama "Wimbi la Rangi ya Machungwa". Wafuasi hao walikuwa wamevalia sare zenye rangi ya chama chake huko katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo jana Jumanne. 

Andre Rajoelina 

Wapiga kura katika kisiwa hicho cha Madagascar kinachopatikana katika Bahari ya Hindi tarehe 9 mwezi Novemba mwaka huu watashiriki katika uchaguzi wa Rais; ambapo kwa zaidi ya wiki moja sasa vyama vya upinzani kisiwani humo vimekuwa vikiandamana dhidi ya kile vilichokitaja kuwa 'Mapinduzi ya Kitaasisi" yenye lengo la kumbakisha madarakani Rajoelina.   

Kampenzi za uchaguzi za Rajoelina alizozizindua jana Jumanne zinaashiria kuanza kwa kipindi cha kampeni kuu za uchaguzi huko Madagascar, hata hivyo wagombea 11 kati ya 13 wa kiti cha urais wamesema kuwa hawatafanya kampeni ikiwa ni ishara ya kubainisha malalamiko yao hadi hapo matakwa yao yatakapopatiwa ufumbuzi. 

Inafaa kuashiria hapa kuwa, Andre Rajoelina mweye miaka 49 alijiuzulu mwezi uliopita kwa mujibu wa katiba ili kugombea tena urais.

 

Tags