Macron: Ufaransa na washirika wake wangeweza kuzuia mauaji ya kimbari ya Rwanda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i110282-macron_ufaransa_na_washirika_wake_wangeweza_kuzuia_mauaji_ya_kimbari_ya_rwanda
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jana Alhamisi alieleza kuwa Ufaransa na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo. Weledi wa mambo wametaja matamshi haya ya Macron kuwa tangazo kali la kuungama kabla ya Rwanda kuadhimisha kutimia miaka 30 tangu nchi hiyo ikumbwe na mauaji ya kimbari ambapo Watutsi na wahutu wenye misimamo ya wastani zaidi ya laki nane waliuawa.
(last modified 2025-11-05T10:50:24+00:00 )
Apr 05, 2024 07:51 UTC
  • Macron: Ufaransa na washirika wake wangeweza kuzuia mauaji ya kimbari ya Rwanda

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jana Alhamisi alieleza kuwa Ufaransa na washirika wake wangeweza kukomesha mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 lakini hawakuwa na nia ya kufanya hivyo. Weledi wa mambo wametaja matamshi haya ya Macron kuwa tangazo kali la kuungama kabla ya Rwanda kuadhimisha kutimia miaka 30 tangu nchi hiyo ikumbwe na mauaji ya kimbari ambapo Watutsi na wahutu wenye misimamo ya wastani zaidi ya laki nane waliuawa.

Ofisi ya Macrom imesema katika taarifa yake kuwa Rais wa Ufaransa ataachia video katika mtandao wa kijamii siku ya Jumapili ambapo Rwanda itaadhimisha miaka 30 tangu kujiri mauaji ya kimbari nchini humo. 

Katika video hiyo, Macron ameeleza kuwa "Ufaransa, ambayo pamoja na washirika wake wa Magharibi na Afrika ingeweza kuzuia mauaji ya halaiki lakini haikuwa na nia ya kufanya hivyo. Katika video hiyo, Rais Emmanuel Macron ameeleza kuwa, Ufaransa na  washirika wake wa Magharibi na Afrika ambayo ingeweza kuzuia kujiri mauaji ya kimbari ya Rwannda ilikosa nia ya kufanya hivyo.”

Kutimia miaka 30 mwaka huu tangu kujiri mauaji ya kimbari Rwanda mwaka 1994 

Akiwa ziarani  mwaka 2021 katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika, Macron alikiri kuhusu dhima inayobeba Ufaransa katika mauaji ya kimbari yaliyopelekea watu zaidi ya laki nane kuuawa wengi wao wakiwa ni Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani waliojaribu kuwalinda.