Apr 24, 2024 02:32 UTC
  • Kushindwa njama za Marekani za kutaka kuendelea kuwa na uwepo wa kijeshi nchini Niger

Baada ya kugonga mwamba mazungumzo ya kisiasa ya Marekani ya kudumisha uwepo wake wa kijeshi nchini Niger, kwa mara nyingine tena raia katika nchi hiyo ya Kiafrika wametoa mwito wa kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani katika nchi yao kwa kufanya maandamano mbele ya kambi ya kijeshi ya Marekani kaskazini mwa Niger.

Ali Lamine Zeine Waziri Mkuu wa Niger na Kurt Campbell, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, walikubaliana juu ya kuandaa jedwali la kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Niger. Kwa mujibu wa maafisa husika, katika majuma ya hivi karibuni wanadiplomasia wa Kimarekani walikuwa wakifuatilia kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa, makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na serikali ya Nigeria yanahiifadhiwa na kubakia. Hata hivyo hawakufanikiiwa kufikia malengo yao.

Mwezi uliopita, serikali ya Niger ilitangaza kuwa, imebatilisha ghafla makubaliano ya kijeshi ambayo yaliruhusu wanajeshi na wafanyakazi wa kiraia wa Idara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon kuwepo kwenye ardhi ya nchi hiyo.

Wanajeshi wa Marekani walioko Niger walizutendaji wao ulizimwa msimu uliopita wa kiangazi baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani rais wa nchi hiyo, Mohamed Bazoum na kuingia madarakani utawala wa kijeshi.

Niger imekuwa makao ya kambi kubwa ya anga ya Marekani katika mji wa Agadez ulioko kilomita zipatazo 920 kutoka mji mkuu Niamey, ambayo Washington imekuwa ikiitumia kwa safari za upelelezi za ndege zake zinazobeba rubani na zisizo na rubani na kwa ajili ya shughuli nyinginezo. Marekani imewekeza pia mamia ya mamilioni ya dola kwa ajili ya utoaji mafunzo kwa jeshi la Niger tangu ilipoanza operesheni zake za kijeshi nchini humo mwaka 2013.

Maandamano ya wananchi wa Niger ya kutaka kuondoka nchini mwao wanajeshi wa Marekani

 

Hatua hiyo ya kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Niger ambayo ilikuwa ikitarajiwa na kungojewa kwa muda mrefu inaashiria mafanikio mapya ya kikanda kwa Russia, ambayo imeongeza harakati zake za kujizatiti barani Afrika na kuunga mkono watawala wa kijeshi katika nchi jirani za Mali na Burkina Faso.

Julai 26 mwaka jana (2023), kikosi cha gadii ya Rais wa Niger vilimkamata rais wa nchi hiyo, Mohammad Bazoum, ndani ya ikulu ya rais, na kisha kumwondoa katika nafasi yake. Vikosi hivyo pia vilimteua Jenerali Abdourahamane Tchiani, kama mkuu wa baraza la mpito la nchi hiyo mnamo Julai 28.

Katika mapinduzi ya Niger, kilichowakera na kuwashangaza wengi wa viongozi na wanajeshi wa Marekani ni kuwepo kwa Jenerali Musa Salo Parmo miongoni mwa waliopanga mapinduzi, ambaye aliungwa mkono na jeshi la Marekani kwa zaidi ya miaka 30.

Vikosi vya Marekani barani Afrika vilikabiliwa na mshtuko mwingine wiki iliyopita wakati mamlaka ya Chad ilipotishia kufuta Makubaliano ya Hali ya Majeshi, yanayojulikana kama SOFA. Mkataba wa SOFA huamua sheria na masharti ambayo jeshi la Marekani linaweza kufanya kazi nchini Chad.

Ingawa makubaliano haya hayakuamuru moja kwa moja jeshi la Marekani kuondoka Chad, lakini kwa mujibu wa maafisa wa Washington, vikosi vyote vya Marekani lazima viondoke katika kambi ya Ufaransa iliyoko katika mji mkuu wa nchi hiyo, N'Djamena.

Takwa la Niger la kusitisha uhusiano wa kijeshi na Marekani limetolewa kufuatia kuondolewa kwa wanajeshi wa Ufaransa katika nchi hiyo. Makubaliano ya kijeshi kati ya Marekani na Niger yanajumuisha kipengele muhimu cha kile kinachoitwa mkakati wa Marekani wa kupambana na ugaidi.

Makubaliano hayo yaliwezesha kuwepo kwa jeshi la Marekani kupitia kambi ya 101 ya Anga huko Niamey, mji mkuu wa Niger, na Kambi ya 201 ya Anga karibu na Agadez, iliyoko kusini magharibi mwa Niamey.

Ndege ya kivita ya Marekani ikiwa katika kituo cha kijeshi cha Agadez nchini Niger

 

Kundi la Wamarekani waliotumwa Niger wamewekwa katika Kambi ya 201 ya Jeshi la Anga la Marekani. Kambi ya anga ya 201 ni kituo cha kijeshi cha miaka 6 kilichogharimu dola milioni 110 na ambacho kiko katika jangwa la kaskazini mwa nchi hii. Lakini tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka jana, jeshi halijafanya kazi katika kambi hiyo na ndege zake nyingi zisizo na rubani za MQ-9 Reaper zimezuiwa isipokuwa operesheni ya ufuatiliaji ili kulinda wanajeshi wa Marekani.

Majukumu ya kijeshi ya Marekani na Ufaransa barani Afrika hayajawa na matunda ya maana katika kuboresha hali ya usalama ya nchi mwenyeji. Wakati huo huo, mafanikio katika mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo hilo yametokana hasa na vikundi vya kijeshi vya kimataifa vinavyojumuisha vitengo vya kijeshi vya Niger, Nigeria, Chad, Cameroon na Benin.

Kufukuzwa kwa wanajeshi wa Marekani na nchi zingine za magharibi kutoka Afrika, kama ambavyo hilo linachukuliwa kuwa janga kwa nchi hizi, wakati huo huo linatoa fursa mpya za kuimarisha uwepo wa washindani wa kimataifa wa nchi hizi, kama vile China na Russia, ambazo zinajaribu kupanua ushawishi wao katika eneo.

Kufuatia kusitishwa kwa ushirikiano wa kijeshi na usalama kati ya Marekani na Niger, wataalamu wa kijeshi wa Russia walielekea Niger kwa ajili ya kutoa mafunzo ya mapigano na kuanzisha mfumo wa ulinzi wa anga katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Kabla ya kuwasili kwa wakufunzi wa kijeshi wa Urusi, kulifanyika mazungumzo ya simu kati ya Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais Abdul Rahman Tchiani wa Baraza la Kitaifa la Niger.

Katika miaka ya hivi karibuni, Moscow imekuwa ikipanua ushawishi wake barani Afrika na kuunda ushirikiano na viongozi wa nchi za Kiafrika. Kwa upande mmoja, hii ni kwa sababu ya uwepo wa rasilimali nyingi katika bara la Afrika, na kwa upande mwingine, kwa sababu Russia, haswa baada ya vita vya Ukraine, inataka kuonyesha kuwa haijatengwa na ina uwezo wa kupanua uhusiano washirika wapya barani Afrika.

Tags