Sudan kuanza mazungumzo ya usitishaji vita
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i12979-sudan_kuanza_mazungumzo_ya_usitishaji_vita
Mazungumzo yenye lengo la kufanikisha usitishaji vita wa kudumu katika mikoa mitatu ya Sudan iliyoathiriwa na mapigano yameanza Jumanne wiki hii siku moja baada ya muungano wa upinzani kusaini ramani ya njia ili kuhitimisha uhasama na kufikia suluhu ya kisiasa.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Aug 10, 2016 03:27 UTC
  • Mazungumzo ya amani Sudan
    Mazungumzo ya amani Sudan

Mazungumzo yenye lengo la kufanikisha usitishaji vita wa kudumu katika mikoa mitatu ya Sudan iliyoathiriwa na mapigano yameanza Jumanne wiki hii siku moja baada ya muungano wa upinzani kusaini ramani ya njia ili kuhitimisha uhasama na kufikia suluhu ya kisiasa.

Mapigano yamekuwa yakijiri kati ya jeshi la Sudan na waasi katika mikoa ya kusini ya Kordofan na Blue Nile tangu mwaka 2011, baada ya Sudan Kusini kutangaza kujitenga na upande wa kaskazini.

Ramani hiyo ya njia iliyosimamiwa na Umoja wa Afrika (AU) imeashiria kwa mara ya kwanza suala la kutiwa saini kati ya makundi makuu ya upinzani na serikali ya Khartoum tangu kuzuka mapigano katika mikoa hiyo mwaka 2011.

Mikoa iliyoathiriwa na vita Sudan

Makubaliano hayo yanatoa fursa ya kufikiwa usitishaji vita wa kudumu, kuanza mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali, waasi na makundi ya kisiasa na pia kuruhusu operesheni za kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu kwa raia walioathirika na mapigano.