Libya yataka kuzidishwa ushirikiano wa kiusalama kati yake na Ufaransa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16237-libya_yataka_kuzidishwa_ushirikiano_wa_kiusalama_kati_yake_na_ufaransa
Libya imetaka kuzidishwa ushirikiano wa kiusalama na kijeshi kati yake na Ufaransa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 28, 2016 04:04 UTC
  • Libya yataka kuzidishwa ushirikiano wa kiusalama kati yake na Ufaransa

Libya imetaka kuzidishwa ushirikiano wa kiusalama na kijeshi kati yake na Ufaransa.

Fayyez al Siraj Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amesema kuwa nchi mbili hizo zimekubaliana kushirikiana kiusalama na kijeshi. Siraj ameyaeleza hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Paris akiwa na Rais wa Ufaransa Francois Hollande. 

Rais wa Ufaransa Francois Hollande (kushoto) akimlaki Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa mjini Paris 

Al Siraj ameeleza kuwa suala la mapambano dhidi ya ugaidi ni moja ya kadhia zenye umuhimu mkubwa iliyogubika mazungumzo kati yake na Rais wa Ufaransa na kwamba vita dhidi ya ugaidi ni suala linaloihusu Libya na jamii ya kimataifa pia. Rais wa Ufaransa na Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya wamejadili pia suala la wahamiaji haramu na jitihada zinazotekelezwa kwa minajili ya kukabiliana na suala hilo; ukiwemo usimamizi wa mipaka na kuamiliana na ongezeko la wimbi la wakimbizi.