Jaribio la mapinduzi lililoshindwa nchini Burkina Faso
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17932-jaribio_la_mapinduzi_lililoshindwa_nchini_burkina_faso
Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa imefichua na kusambaratisha njama za kutaka kuipindua serikali hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 22, 2016 08:56 UTC
  • Jaribio la mapinduzi lililoshindwa nchini Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa imefichua na kusambaratisha njama za kutaka kuipindua serikali hiyo.

Simon Compaore Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burkina Faso amesisitiza kwenye mkutano na waandishi wa habari huko Ouagadougou mji mkuu wa nchi hiyo kuwa kundi moja la watu 30 lilipanga njama za kuipindua serikali tarehe 18 mwezi huu, hata hivyo walikamatwa na askari usalama. Watu hao 30 walipanga kuwaachia huru wafungwa wale ambao walishiriki katika jaribio la mapinduzi lililofeli la mwezi Septemba mwaka jana; na kisha watelekeze shambulizi katika ikulu ya Rais. Watekelezaji wa jaribio hilo ni wanawajumuisha waitifaki na shakhsia watiifu kwa Blaisse Compaore Rais wa zamani wa Burkina Fasso; ambao walikusudia kuipindua serikali ili kumrejesha yeye madarakani.  

Blaisse Compaore ambaye alisalia madarakani kwa miaka 27 alijaribu kuifanyia mabadiliko katiba ya Bukina Faso ili aendelee kuiongoza nchi hiyo, mwezi Oktoba mwaka 2014 alilazimika kujiuzulu kiti cha rais na kisha akakimbilia nchini Kodivaa. Hivi sasa pia Blaisse Compaore anaishi uhamishoni nchini humo. Mapambano ya ukombozi ya wananchi na maandamano ya mitaani ya wapinzani huko Ouagadougou mji mkuu wa Burkina Faso miaka miwili iliyopita yalipelekea kujiuzulu Rais Blaisse Compaore. Pamoja na hayo yote, waitifaki na maafisa wa jeshi wanajeshi waliokuwa wakiunga mkono udikteta ndani ya jeshi la Burkina Faso tarehe 17 Septemba mwaka jana walivishambulia vituo vya redio na televisheni vya serikali na kuwatangazia wananchi kwamba mapinduzi ya kijeshi yametokea nchini humo.

 

Blaisse Compaore, Rais wa zamani wa Burkina Faso aliyelazimika kujiuzulu kufuatia maandamano ya wananchi

Njama za mapinduzi mnamo Oktoba 18 huko Burkina Faso ilikuwa ni jitihada za mara ya pili za kuing'oa madarakani serikali ya mpito ya nchi hiyo ambayo ndiyo inayoiongoza nchi hadi kufikia sasa tangu kuangushwa serikali ya kidikteta nchini humo. Wakati huo huo vyama vinane vya upinzani nchini humo katikati ya mwezi Oktoba vilitangaza kuasisi muungano wao wa kisiasa kwa jina la "Muungano kwa ajili ya Demokrasia na Suluhu ya KItaifa." Wakuu wa muungano huo  ambao unakijumuisha chama tawala cha zamani cha nchini Burkina Faso cha Congresi kwa ajili ya Demokrasia na Maendeleo pia, walitaka kufanya mazungumzo na serikali ya mpito ya nchi hiyo. Kufichuliwa njama za kutaka kuipindua serikali kunaashiria kwamba juhudi za wakuu wa muuungano huo wa vyama vya kisiasa huko Burkina Faso vyenye mfungamano wa kisiasa na dikteta wa zamani wa nchi hiyo, zimefeli katika mazungumzo kati yao na serikali hiyo ya mpito. 

Pamoja na kuwa katika miaka ya hivi karibuni majaribio ya mapinduzi yamekuwa yakitokea katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika, lakini weledi wengi wa mambo wanaamini kuwa zama zile ambapo bara hilo lilipata umashuhuri kwa kufahamika kama "Bara la Mapinduzi" zimepitwa na wakati. Wafanya mapinduzi hao ambao wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya maafisa jeshini ili kuipindua serikali iliyoko madarakani, wamekuwa wakilitaja lengo la kufanya hivyo kuwa ni kutaka kuzuia kutokea hofu na hali ya wasiwasi na kugawanyika nchi. Mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Guinea Bissau, Niger na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika miaka ya hivi karibuni pia yalitangazwa kwa wananchi kuwa yalifanyika kwa malengo kama hayo. Mapinduzi hayo ambayo hayakuungwa mkono na wanaharakati wa kisiasa na vyama katika nchi za Kiafrika yalifikia ukomo kwa kutiwa mbaroni wapangaji wake. Amma wafanya mapinduzi ambao wameazia kuchukua madaraka kwa kutumia nguvu, siku zote wamekuwa wakilaaniwa vikali na Umoja wa Afrika na taasisi za kieneo. Wakuu wa Umoja wa Afrika wanaziunga mkono serikali za kidemokrasia za Kiafrika na kuwapinga wale wenye lengo la kuzipindua serikali hizo; na kamwe hazijatoa fursa kwa mirengo hiyo kuingia madarakani. Kwa hiyo kushindwa majaribio mawili ya mapinduzi ya hivi karibuni huko Burkina Faso kunatilia mkazo madai hayo. 

Wananchi wanaoipinga serikali ya Burkina Faso walipokabiliana na polisi wa kuzuia ghasia mwaka juzi 2014