Jeshi Nigeria laua Waislamu 100 wa madhehebu ya Shia mjini Kano
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19468-jeshi_nigeria_laua_waislamu_100_wa_madhehebu_ya_shia_mjini_kano
Waislamu wasiopungua 100 wa madhehebu ya Shia wameuawa leo nchini Nigeria kwa kupigwa risasi na jeshi la nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 14, 2016 12:46 UTC
  • Jeshi Nigeria laua Waislamu 100 wa madhehebu ya Shia mjini Kano

Waislamu wasiopungua 100 wa madhehebu ya Shia wameuawa leo nchini Nigeria kwa kupigwa risasi na jeshi la nchi hiyo.

Waislamu hao wameuawa walipokuwa katika shughuli ya kidini nje kidogo ya mji wa Kano ulioko kaskazini mwa Nigeria. Waislamu wengine kadhaa wamejeruhiwa.

Kamishna wa polisi katika mji huo, Rabiu Yusuf amedai kuwa, mauaji hayo yametokea baada ya Waislamu hao kuwashambulia polisi kwa kutumia silaha baridi kama mapanga na mishale. Hata hivyo watu walioshuhudia wanakadhibisha madai hayo na kusema, polisi waliwashambulia Waislamu hao waliokuwa katika maandamano ya amani.

Waislamu wa Nigeria wakiwa katika shughuli ya kidini

Disemba mwaka jana jeshi la Nigeria lilishambulia kituo cha kidini cha Baqiyatullah katika mji wa Zaria na kuua mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia. Jeshi la Nigeria pia lilimtia nguvuni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe na hadi sasa wanashikiliwa katika korokoro ya nchi hiyo.