Nov 15, 2016 02:51 UTC
  • Al Sisi: Mfalme wa Saudia aiombe radhi Misri

Rais wa Misri amesema kuwa anataka Mfalme wa Saudi Arabia aiombe radhi Misri kama sharti la kuweza kuzisuluhisha Cairo na Riyadh.

Rais Abdel Fattah al Sisi wa Misri amesema kuwa Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia anapaswa kuiomba radhi nchi yake kama sharti la kusuluhisha hitilafu zilizopo kati ya Cairo na Riyadh. Rais wa Misri amezungumza na Mwana Mfalme wa Abu Dhabi, Mohammed bin Zaid al Nahyan katika ikulu ya al Itihadiya mjini Cairo kuhusu hitilafu zilizopo kati ya Cairo na Riyadh.

Rais al Sisi wa Misri akimlaki Mwana Mfalme wa Abu Dhabi Sheikh Mohammed bin Zaid al Nahyan

Hitilafu kati ya Cairo na Riyadh zimeshadidi tangu wiki mbili zilizopita. Kabla ya hapo, baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza kuwa kunafanyika jitihada kubwa za kisiasa na mashauriano kati ya nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi kwa minajili ya kurejesha uhusiano wa kawaida kati ya Cairo na Riyadh.

Karibu miezi miwili imepita sasa ambapo uhusiano wa Misri na Saudia umeingia dosari baada ya hatua ya Saudi Arabia ya kusimamisha uuzaji wa mafuta kwa Misri licha ya mapatano yaliyofikiwa kabla kati ya nchi mbili hizo ili kufufua uchumi wa Misri.

Tags