Kundi la ash Shabab lashambulia kusini mwa Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20989-kundi_la_ash_shabab_lashambulia_kusini_mwa_somalia
Watu wanne wameuawa baada ya kundi la kigaidi la ash Shabab kushambulia eneo moja la kusini mwa Somalia.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 08, 2016 04:08 UTC
  • Kundi la ash Shabab lashambulia kusini mwa Somalia

Watu wanne wameuawa baada ya kundi la kigaidi la ash Shabab kushambulia eneo moja la kusini mwa Somalia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, wanamgambo wa ash Shabab walifanya shambulio hilo jana Jumatano katika eneo la Juba al Sufli, kusini mwa Somalia ambako kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM kina wanajeshi wake. Habari zinasema kuwa, wanajeshi wanne wa AMISOM wameuawa kwenye shambulio hilo.

Kundi la ash Shabab ambalo ni tawi la mtandao wa kigaidi wa al Qaida, lilianzisha mashambulizi mwaka 2007 kwa lengo la kuipundua serikali ya Somalia na mwaka 2011 likafanikiwa kudhibiti maeneo mengi ya nchi hiyo.

 

Licha ya kwamba kundi la ash Shabab limefukuzwa mjini Mogadishu tangu miaka mitano iliyopita, lakini bado linafanya mashambulizi ya hapa na pale dhidi ya askari wa serikali na wanajeshi pamoja na raia.

Umoja wa Afrika umetuma wanajeshi wake nchini Somalia kwa jina la kikosi cha kulinda amani cha AMISOM ili kukabiliana na ash Shabab na limefanikiwa kwa kiasi fulani kulidhibiti kundi hilo. Kenya ambayo ina mpaka na Somalia na ambayo imeshuhudia mashambulizi mengi ya kigaidi ya kundi hilo, nayo ina wanajeshi wake nchini Somalia.