Trump aishurutisha Misri kuakhirisha azimio la UN dhidi ya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21997-trump_aishurutisha_misri_kuakhirisha_azimio_la_un_dhidi_ya_israel
Rais mteule wa Marekani amempigia simu Rais wa Misri na kuitaka Cairo iakhihirshe uwasilishaji wa rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 23, 2016 12:54 UTC
  • Trump aishurutisha Misri kuakhirisha azimio la UN dhidi ya Israel

Rais mteule wa Marekani amempigia simu Rais wa Misri na kuitaka Cairo iakhihirshe uwasilishaji wa rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi imesema kuwa, viongozi hao wawili (yaani yeye Sisi na Donald Trump) wameafikiana kuwa Cairo isiwasilishe rasimu hiyo iliyoandaa dhidi ya Israel kwa sasa, na kwamba uwasilishaji huo ufanyike baadaye.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Rais mteule wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Misri Abdul Fattah al-Sisi wamekubaliana kuwa, kuna haja ya rasimu hiyo kutowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kupigiwa kura, ili kutoa fursa kwa utawala mpya wa Washington eti kushughulikia kadhia ya Palestina kwa kuzihuhusisha pande zote na kuja na suluhisho la kudumu.

Trump na Sisi walipokutana mjini New York Septemba 19, 2016

Hapo jana Trump alitaka kupigiwa kura ya turufu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.

Donald Trump alisema: "Kwa muda mrefu Marekani imekuwa ikisisitiza kuwa, amani kati ya Israel na Palestina itapatikana tu kwa njia ya mazungumzo na wala sio kwa masharti na mashinikizo ya Umoja wa Mataifa."

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitazamiwa kupigia kura rasimu ya azimio hilo iliyoandaliwa na Misri jana Alkhamisi.

Kufuatia hatua ya Misri ya kusuasua katika uwasilishaji wa rasimu ya azimio hilo baada kushinikizwa na Marekani, New Zealand, Venezuela, Malaysia na Senegal zimeipa Cairo hadi leo saa sita usiku iwe imewasilisha rasimu hiyo, vinginevyo nchi hizo zitaandaa rasimu zao wenyewe.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa