Amani na mapatano ya kitaifa, kipaumbele cha wakuu wa Afrika mwaka 2017
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22624-amani_na_mapatano_ya_kitaifa_kipaumbele_cha_wakuu_wa_afrika_mwaka_2017
Viongozi wa nchi za Kiafrika wamesema kuwa siasa zao kwa mwaka mpya wa 2017 zinatoa kipaumbele kwa suala la kurejesha amani na kupatikana suluhu ya kitaifa barani humo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 02, 2017 00:49 UTC
  • Amani na mapatano ya kitaifa, kipaumbele cha wakuu wa Afrika mwaka 2017

Viongozi wa nchi za Kiafrika wamesema kuwa siasa zao kwa mwaka mpya wa 2017 zinatoa kipaumbele kwa suala la kurejesha amani na kupatikana suluhu ya kitaifa barani humo.

Wakuu wa nchi za Kiafrika sambamba na kuanza mwaka mpya wa 2017 wamesema wanataraji kuwa  vitisho vya ugaidi vitapungua na pia kutapatikana umoja na mapatano ya kitaifa katika nchi za Kiafrika katika mwaka huu wa 2017. Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amezitolea wito pande zote nchini humo kushiriki katika mchakato wa kurejesha amani na uthabiti baada ya kusaini na wapinzani muafaka wa kisiasa wa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Rais Joseph Kabila wa Congo DR ataondoka madarakni mwaka huu wa 2017 

Akiwahutubia wananchi wa Kongo Brazaville, Rais Denis Sassou Ngueso wa nchi hiyo ametaka mwaka mpya wa 2017 uwe ni mwaka wa ukweli na kupambana na matatizo hasa ya kiuchumi yanayosababishwa na kushuka bei ya mafuta. Naye Rais Paul Biya wa Cameroon ametaka kufanyike juhudi za kuendesha vita dhidi ya ugaidi na misimamo mikali. 

Wakati huo huo Rais Faustin Archange Teodore wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amewatumia wananchi salamu za mwaka mpya na kuwataka kuwa na umoja na kwamba serikali inafanya juhudi za kufufua uchumi na kufanikisha mapatano ya kitaifa. Rais Mahamadou Issoufou wa Niger kwa upande wake ametangaza azma thabiti ya nchi yake ya kuendesha vita dhidi ya kundi la kigaidi la Boko Haram na kuwataka vijana wa nchi  hiyo waliojiunga na kundi hilo waweke chini silaha zao na wasaidie kuimarisha hali ya usalama na ya kiuchumi ya nchi hiyo katika mwaka huu mpya. 

Kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo limefanya hujuma na jinai chungu nzima dhidi ya raia wa Nigeria na wa nchi nyingine za Magharibi mwa Afrika