Feb 10, 2017 15:35 UTC
  • Gadi ya Taifa yaundwa katika mji mkuu wa Libya,Tripoli

Kikosi cha jeshi kwa jina la "Gadi ya Taifa" chenye mfungamano na Serikali ya Wokovu ya Libya kimeasisiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.

Gadi ya Taifa ya Libya yenye mfungamano na Serikali ya Wokovu wa Kitaifa inayoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar imetoa taarifa ikieleza kuwa, kikosi hicho kimeanza shughuli zake jana Alhamisi mjini Tripoli  kwa ajili ya kushiriki katika juhudi za kurejesha amani na kushirikiana na taasisi zote za usalama. 

Taarifa ya Gadi ya Taifa la Libya imeongeza kuwa, ina mpango wa kuanzisha taasisi ya kitaifa iliyombali na mivutano ya kisiasa, vyama na makundi ya kikabila kwa lengo la kupambana na vitendo vyote vya uhalifu na ugaidi ambazo zinaathiri usalama wa taifa na raia wa Libya. Taarifa hiyo imesema kwamba gadi ya Taifa la Libya imeazimia kuzuia kuenea silaha haramu na kuzilinda balozi za nchi za nje na jumbe za kidiplomasia sambamba na kuwadhaminia usalama raia wa nchi za kigeni.

Askari wa serikali ya Libya katika mapambano na magaidi

Mji mkuu wa Libya Tripoli umekuwa uwanja wa mapigano makali kati ya wapiganaji wa Serikali ya Wokovu inayoongozwa na Waziri Mkuu Fayyez al Siraj na makundi yanayobeba silaha. 

Tags