Jeshi la Nigeria: Tutapeleka kikosi maalumu cha polisi katika maeneo yenye machafuko
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25534-jeshi_la_nigeria_tutapeleka_kikosi_maalumu_cha_polisi_katika_maeneo_yenye_machafuko
Jeshi la polisi nchini Nigeria limetangaza azma yake ya kupeleka kikosi maalumu cha polisi kwa ajili ya kusimamia amani katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2017 09:45 UTC
  • Jeshi la Nigeria: Tutapeleka kikosi maalumu cha polisi katika maeneo yenye machafuko

Jeshi la polisi nchini Nigeria limetangaza azma yake ya kupeleka kikosi maalumu cha polisi kwa ajili ya kusimamia amani katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Hayo yamesemwa na Aghole Abeh, kamanda wa polisi wa jimbo la Kaduna nchini humo na kuongeza kuwa, katika juhudi za kuhitimisha mgogoro wa ndani na kuzuia kuenea vitendo vya ukatili kutoka jimbo hilo kwenda maeneo mengine ya Nigeria, jeshi hilo litatuma kikosi maalumu huko kaskazini mashariki mwa nchi. Aidha Abeh amewataka raia wa nchi hiyo kuwa waelewa kuliko kipindi kingine chochote kile hususan katika kukabiliana na machafuko ili katika harakati hizo wananchi wasipoteze maisha yao.

Sehemu ya kikosi maalumu cha polisi Nigeria

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na shirika la taifa la kukabiliana na migogoro nchini Nigeria, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi sasa zaidi ya watu 200 wameuawa katika mapigano huko katika jimbo la Kaduna. Kadhalika Aghole Abeh, kamanda wa polisi la jimbo la Kaduna ameelezea kuanza kuruka ndege zisizo na rubani katika anga ya jimbo hilo kwa ajili ya kufuatilia hali ya mambo.

Sehemu ya wanachama wa genge la ukufurishaji la Boko Haram

Inafaa kuashiria hapa kwamba, tangu mwaka 2009 Nigeria imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya wanachama wa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram huku serikali nao kwa upande wao wakipoteza nguvukazi nyingi katika kukabiliana na kundi hilo pamoja na makundi mengine hatari.