Magaidi watatu wakufurishaji wauawa Sinai, Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31844-magaidi_watatu_wakufurishaji_wauawa_sinai_misri
Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuuawa magaidi watatu wakufurishaji katikati ya Rasi ya Sinai, kaskazini mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2017 10:38 UTC
  • Magaidi watatu wakufurishaji wauawa Sinai, Misri

Jeshi la Misri limetangaza habari ya kuuawa magaidi watatu wakufurishaji katikati ya Rasi ya Sinai, kaskazini mwa nchi hiyo.

Shirika la habari la Ufaransa limelinukuu jeshi la Misri likitangaza leo kuwa, askari wa jeshi hilo wamefanikiwa kuangamiza magaidi watatu na kumtia mbaroni mwengine mmoja.

Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kuwa, askari wa jeshi hilo wameshambulia maficho ya magaidi katika operesheni ya kuyasafisha maeneo hayo na uwepo wa magaidi wenye misimamo mikali na kufanikiwa kuteketeza maghala matano ya silaha za magaidi hao.

Hivi sasa serikali ya Misri imeshadidisha mashambulizi yake kwa shabaha ya kuwafuta kabisa magaidi wenye misimamo mikali ambao wana mfungamano na genge la kigaidi la Daesh, na ambao wana maficho yao katika Rasi ya Sinai, kaskazini mwa Misri.

Si

Wanajeshi wa Misri katika operesheni ya kupambana na mgaidi katika Rasi ya Sinai

 

Wanajeshi wasiopungua 21 wa Misri waliuawa kwenye shambulizi la kigaidi lililofanywa na magaidi hao katika mkoa huo wa Sinai siku ya Ijumaa ya tarehe 7 ya mwezi huu wa Julai. Genge la kigaidi la Daesh lilitangaza kuhusika na shambulio hilo. 

Siku ya pili yake yaani Jumamosi ya tarehe 8 Julai, jeshi la Misri lilitangaza kuwa, limewaangamiza magaidi 16 waliohusika na shambulizi hilo. 

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri ilisema kuwa, magaidi hao 16 waliuawa katika mkoa wa Ismailia kutokana na kuhusika na shambulio lililopelekea wanajeshi wasiopungua 21 wa serikali ya Misri kuuawa siku ya Ijumaa.