Watu wanne wauawa katika shambulizi la roketi Sinai, Misri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i36077-watu_wanne_wauawa_katika_shambulizi_la_roketi_sinai_misri
Raia wanne wamepoteza maisha katika shambulizi la roketi lililotokea leo Jumanne katika mji wa Arish, katika Peninsula ya Sinai nchini Misri.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Oct 31, 2017 10:17 UTC
  • Watu wanne wauawa katika shambulizi la roketi Sinai, Misri

Raia wanne wamepoteza maisha katika shambulizi la roketi lililotokea leo Jumanne katika mji wa Arish, katika Peninsula ya Sinai nchini Misri.

Afisa wa serikali ambaye hakutaka kutaja jina lake ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, mtu mmoja aidha amejeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo lililolenga trekta.

Habari zinasema kuwa, hujuma hiyo imetekelezwa na moja ya magenge ya kigaidi na kitakfiri yenye mafungamano na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).

Haya yanajiri wiki mbili baada ya Jeshi la Misri kutangaza habari ya kuwaua wanachama 24 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) katika eneo la Sinai. kaskazini mwa nchi.

Magaidi wa Daesh eneo la Sinai

Eneo hilo la kaskazini mwa Misri limekuwa uwanja wa mashambulizi ya makundi yenye silaha kwa miaka kadhaa sasa. 

Eneo hilo halijawahi kuwa na utulivu tangu magenge ya kigaidi yaanzishe harakati zao mwaka 2013, baada ya jeshi la Misri kumuondoa madarakani kwa nguvu Mohamed Morsi, rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri.