Weledi wa mambo: Safari ya Rais Macron nchini Tunisia imeambulia patupu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i39835-weledi_wa_mambo_safari_ya_rais_macron_nchini_tunisia_imeambulia_patupu
Weledi wa masuala ya kisiasa wameitaja safari ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa nchini Tunisia kuwa imeambulia patupu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 03, 2018 00:08 UTC
  • Weledi wa mambo: Safari ya Rais Macron nchini Tunisia imeambulia patupu

Weledi wa masuala ya kisiasa wameitaja safari ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa nchini Tunisia kuwa imeambulia patupu.

Toleo la mtandaoni la gazeti la al-Arab limeandika kwamba safari ya Rais Macron nchini Tunisia imesababisha Watunisia wengi kukata tamaa kwa kuwa safari hiyo haikuwa na manufaa yoyote ya kiuchumi kwao. Weledi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba, safari ya rais huyo wa Ufaransa nchini Tunisia ilikuwa ya kawaida sana na kwamba haikuwa na tofauti yoyote na safari za viongozi wengine wa zamani wa serikali ya Paris nchini mwao.

Bendera za Tunisia na Ufaransa

Abdul-Wahhab Taqiyah, mtaalamu wa masuala ya kiuchumi wa Tunisia amesema kuwa, ni suala lililo mbali kwa Wafaransa na katika hali ya hivi sasa kuwa na mipango mikubwa ya uwekezaji na kwa ajili hiyo, ni suala lisilo sahihi kuwa na matarajio yoyote na Ufaransa. Kwa upande wake Mustafa Abdul-Kabir, mwanaharakati wa masuala ya sheria nchini Tunisia amesema kuwa Rais Emmanuel Macron amekiri kwamba siasa za Ufaransa ni haribifu katika eneo la kaskazini mwa Afrika ikiwemo Tunisia na Libya. Hata hivyo kukiri huko hakuna maslahi yoyote kwa raia wa nchi hizo za Kiafrika.

Watunisia wakiandamana kulalamikia hali ngumu ya maisha

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa aliwasili mjini Tunis Alkhamisi ya juzi na baada ya hapo alielekea mjini Dakar, Senegal. Ufaransa ina uhusiano wa kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi wa muda mrefu na Tunisia kiasi kwamba Paris inahesabiwa kuwa mshirika mkubwa wa kiuchumi wa Tunis kutokana na kuwa na asilimia 70 ya miamala ya kibiashara na Tunisia.