Ripoti: Saudia na Imarati zilipanga njama ya mapinduzi Tunisia
Vyombo vya habari vya Tunisia vimefuchua kwamba Saudi Arabia na Imarati zilipanga njama ya kuipindua serikali ya nchi hiyo.
Ripoti zinasema kuwa, Saudi Arabia na Imarati zilipanga njama ya kuiondoa madarakani serikali ya Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia lakini njama hiyo imefeli.
Ripoti zimefichua kwamba, Riyadh na Abu Dhabi zilipanga mkakati wa kumuondoa madarakani kiongozi wa sasa wa Tunisia, Beji Caid Essebsi na kumrejesha Zainul Abidin bin Ali aliyeondolewa madarakani kwa mapinduzi ya wananchi na kukimbilia Saudi Arabia.
Habari zimefichua kwamba hadi sasa Saudi Arabia ina matumaini ya kumrejesha madarakani Bin Ali na kwamba ni kwa sababu hiyo ndiyo maana vyombo vya habari vyenye mfungamano na Riyadh vinaeneza uvumi kwamba hali ya watu wa Tunisia katika kipindi cha utawala wa Zainul Abidin bin Ali ilikuwa nzuri kuliko ilivyo kwa sasa.
Kituo cha habari cha Rai Tunisia kimefichua kwamba, Wasaudia na Waimarati wanatumia fedha na ushawishi wa vyombo vya habari kuwashatayarisha wananchi wa Tunisia kwa ajili ya kumrejesha madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Zainul Abidin bin Ali.
Dikteta huyo aliondolewa madarakani katika wimbi la mapinduzi ya wananchi mwaka 2011 na kukimbilia Saudi Arabia.