Muda wa hali ya hatari waongezwa nchini Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41307-muda_wa_hali_ya_hatari_waongezwa_nchini_tunisia
Ofisi ya Rais wa Tunisia ilitangaza jana kwamba, muda wa hali ya hatari umeongezwa nchini humo kwa miezi saba mingine. Muda huo ulikuwa unamalizika tarehe 12 mwezi huu wa Machi 2018.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 07, 2018 07:32 UTC
  • Muda wa hali ya hatari waongezwa nchini Tunisia

Ofisi ya Rais wa Tunisia ilitangaza jana kwamba, muda wa hali ya hatari umeongezwa nchini humo kwa miezi saba mingine. Muda huo ulikuwa unamalizika tarehe 12 mwezi huu wa Machi 2018.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo, Rais Mohamed Beji Caid Essebsi wa Tunisia amechukua uamuzi huo baada ya kushauriana na Waziri Mkuu na Spika wa Bunge la nchi hiyo.

Tarehe 10 Februari 2018, Rais wa Tunisia alirefusha pia muda wa hali ya hatari nchini humo kwa mwezi mmoja mwingine.

Sheria ya hali ya hatari ilianza kutekelezwa nchini Tunisia tarehe 24 Novemba 2015 baada ya kutokea shambulio la kigaidi dhidi ya basi moja la askari wa ulinzi wa Rais mjini Tunis. Sheria hiyo imekuwa ikirefushwa mara kwa mara.

Katika shambulio hilo la mwezi Novemba 2015, watu 38 waliuawa wakiwemo maafisa 12 wa polisi. Kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) lilitangaza kuhusika na shambulio hilo.