Maelfu ya watu wakimbia makazi yao Ethiopia
Maelfu ya watu wamelazimika kukimbia makazi yao katika maeneo ya mpaka wa Ethiopia na Somalia kutokana na mapigano makali yanayoendelea katika eneo hilo.
Maafisa wa serikali ya Ethiopia wamesema kuwa, watu wasiopungua laki saba na elfu kumi wamekimbia nyumba na makazi yao kutokana na mapigano na ghasia zinazotawala maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Somalia.
Mapigano hayo makali yaliyoanza mwezi Septemba mwaka jana katika maeneo hayo ya mpakani pia yamesababisha vito vya watu wengi.
Maeneo ya mpaka wa Somalia na Ethiopia yamekuwa uwanja wa ghasia na mapigano kwa karibu miongo miwili miwili. Sababu kuu ya mapigano hayo inatajwa kuwa ni hitilafu za kuainisha mpaka wa nchi hizo mbili.
Katika miaka ya hivi karibuni hitilafu hizo zimezusha mapigano ya kikabila baina ya wakazi wa jimbo la Oromia nchini Ethioopia na makabila ya majimbo ya Somalia yanayokaribia eneo la mpaka wa nchi hizo mbili.