Waziri Mkuu wa Tunisia ampiga kalamu nyekundu Waziri wa Mambo ya Ndani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i45520-waziri_mkuu_wa_tunisia_ampiga_kalamu_nyekundu_waziri_wa_mambo_ya_ndani
Waziri Mkuu wa Tunisia amempiga kalamu nyekundu Waziri wa Mambo ya Ndani bila kutaja sababu ya hatua yake hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 07, 2018 02:47 UTC
  • Waziri Mkuu wa Tunisia ampiga kalamu nyekundu Waziri wa Mambo ya Ndani

Waziri Mkuu wa Tunisia amempiga kalamu nyekundu Waziri wa Mambo ya Ndani bila kutaja sababu ya hatua yake hiyo.

Youssef Chahed, amemvua uongozi Lutfi Barham, katika hali ambayo hadi sasa hakujatajwa sababu yoyote ya hatua hiyo ingawa baadhi ya duru zimeihusisha hatua hiyo na tukio la kuzama boti ya wahajiri karibu na pwani ya kusini mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Kwa mujibu wa baadhi ya duru za habari,  Ghazi al-Jaribi Waziri wa Vyombo vya Mahakama ameteuliwa kushikilia nafasi hiyo. Kabla ya hapo baadhi ya maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo walipigwa kalamu nyekundu kufuatia tukio hilo la kuzama boti ya wahajiri. 

Boti ya wahajiri wakati ikianza kuzama

Wahajiri haramu 35 walipoteza maisha baada ya boti yao kuzama baharini nchini Tunisia huku wengine 67 wakiokolewa katika oparesheni ya gadi ya pwani ya nchi hiyo. Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Tunisia ilisema miongoni mwa wahajiri hao kulikuwa na raia wa kigeni na pia wa Tunisia. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu zaidi ya watu 340 wametiwa mbaroni nchini Tunisia wakati wakijaribu kuhajiri kuelekea Ulaya ambako wanadhani watapata maisha mazuri. Zaidi ya watu 87,000 walihatarisha maisha yao katika safari hizo za baharini za kuogofya, wakijaribu kufika Yemen mwaka jana pekee.