Jul 08, 2018 04:36 UTC
  • WHO: Tishio la ugonjwa wa Ebola limepungua DRC

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa limepunguza kiwango cha tishio la kutokea kwa ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kutoka kiwango cha juu hadi kiwango cha wastani katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Baada ya kuchunguza kiwango cha tishio la afya ya umma inayohusishwa na kutokea kwa ugonjwa huo katika siku za hivi karibuni, shirika hilo lilithibitisha kuwa ugonjwa wa Ebola umedhibitiwa kwa kiwango kikubwa.

Tokea Aprili 1 hadi Julai 3 mwaka 2018 watu 53 waliripotiwa kuambukizwa Ebola katika mkoa wa Equateur huko Jamhuri ya Kdemokrasia ya Congo, ambapo watu 29 walipoteza maisha.

Mgonjwa wa Ebola akipata matibabu

Maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yalianzia katika mji wa Bikoro kwenye mkoa wa Équateur huko kaskazini magharibi mwa DRC na baadaye kuhamia katika mji wa Mbandaka ambao ndio makao makuu ya mkoa huo.

Kuanzia mwishoni mwa mwaka 2013 hadi 2016 ugonjwa huo ulisababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 11 na 300 katika nchi za magharibi mwa Afrika. 

 

Tags