Chama cha Al Nahdha chapinga Youssef Chahed kugombea uchaguzi wa rais
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46857-chama_cha_al_nahdha_chapinga_youssef_chahed_kugombea_uchaguzi_wa_rais
Chama cha Kiislamu nchini Tunisia cha al Nahadha kimepinga Waziri Mkuu wa nchi hiyo kugombea uchaguzi wa rais nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 18, 2018 03:03 UTC
  • Chama cha Al Nahdha chapinga Youssef Chahed kugombea uchaguzi wa rais

Chama cha Kiislamu nchini Tunisia cha al Nahadha kimepinga Waziri Mkuu wa nchi hiyo kugombea uchaguzi wa rais nchini humo.

Chama cha al Nahdha kimetoa taarifa kikimtaka Youssef Chahed Waziri Mkuu wa nchi hiyo aliye na mfungamano na chama cha Nidaa Tunis; chama cha pili kwa ukubwa huko Tunisia kutogembea uchaguzi wa rais wa mwaka kesho. 

Al Nahdha aidha imekosoa utendaji dhaifu wa serikali ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa serikali ya Waziri Mkuu huyo inapasa kutii mchakato wa ufuatiliaji wa marekebisho ya kiuchumi yanayotekelezwa nchini humo. 

Chama cha Kiislamu cha al Nahdha kinachoongozwa na Rashid Ghanoush kinadhibiti viti 69 vya uwakilishi bungeni kati ya jumla ya viti 217 la bunge zima na ni chama kikubwa zaidi ndani ya bunge hilo.  

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia pia amemtahadharisha Waziri wake Mkuu huyo kuhusu hali ya kisiasa na kiuchumi ya nchi hiyo na kueleza kuwa iwapo mgogoro wa kisiasa na kiuchumi utaendelea nchini humo Waziri Mkuu huyo hatokuwa na chaguo jingine ghairi ya kujiuzulu wadhifa huo au kupigiwa upya kura bungeni ya kuwa na imani naye. 

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia 

Waziri Mkuu wa Tunisia Youssef Chahed mwenye umri wa miaka 43 ambaye anahesabiwa kuwa Waziri Mkuu kijana zaidi katika historia ya nchi hiyo kunzia msimu wa baridi kali uliopita amekuwa akikosolewa vikali kuhusu utendaji wa serikali yake katika sekta ya uchumi  na kupelekea hata kukosolewa pia na wanachama wenzake.