Rais wa sasa na wawili wa zamani wa Madagascar kugombea urais
(last modified Sun, 19 Aug 2018 04:09:06 GMT )
Aug 19, 2018 04:09 UTC
  • Rais wa sasa na wawili wa zamani wa Madagascar kugombea urais

Rais wa sasa wa Madagascar na watangulizi wake wawili watachuana katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha rais wa nchi hiyo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 7 Novemba.

Uchaguzi huo ni sehemu ya harakati ya kukomesha mgogoro wa kisiasa unaoisumbua madagascar kwa muda sasa.

Rais Hery Rajaonarimampianina wa Madagascar atachuana na Andry Rajoelina, akiyetwaa madaraka ya nchi mwaka 2009 kupitia njia ya mapinduzi ya jeshi na Marc Ravalomanana aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi hayo. 

Marc Ravalomanana

Mapinduzi hayo ya kijeshi yaliwatia hofu wawekezaji wa kigeni na kuwafanya waondoke nchini Madagascar ambayo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi barani Afrika licha ya kuwa na utajiri wa madini kama dhahabu, cobalt na uraniuam.

Wagombea wengine katika uchaguzi huo ni pamoja na mwanamuziki na mawaziri wakuu wawili wa zamani wa Madagascar.