Wawakilishi wa Nidaa Tounes waendelea kujiuzulu bungeni Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48658-wawakilishi_wa_nidaa_tounes_waendelea_kujiuzulu_bungeni_tunisia
Wabunge wa chama tawala cha Nidaa Tunis nchini Tunisia wanaendelea kujiuzulu nafasi zao katika bunge la nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 08, 2018 09:57 UTC
  • Beji Caid Essebsi anakabiliwa na uasi ndani ya chama tawala Tunisia.
    Beji Caid Essebsi anakabiliwa na uasi ndani ya chama tawala Tunisia.

Wabunge wa chama tawala cha Nidaa Tunis nchini Tunisia wanaendelea kujiuzulu nafasi zao katika bunge la nchi hiyo.

Mohamed Ben Souf aliyekuwa mbunge wa chama cha Nidaa Tounes kinachoongozwa na Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya uwakilishi bungeni na kuifanya idadi ya wabunge wa chama hicho waliojiuzulu hadi sasa  kufikia 20.  

Wabunge wengine wanne wa chama cha Nidaa Tounes  walitangaza kujiuzulu nafasi zao siku chache zilizopita wakilalamikia hatua na misimamo ya upande mmoja ya chama hicho.

Chama cha Nidaa Tounes kimepoteza udhibiti na wingi wa viti katika Bunge la Tunisia kufuatia kujiuzulu kwa wabunge hao. Wabunge hawa wanatazamia kujiunga na mrengo wa Muungano wa Kitaifa unaomuunga mkono Youssef Chahed, Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Hitilafu za kisiasa zimeshika kasi nchini Tunisia katika miezi ya karibuni. Vyama vya upinzani nchini humo vimemtaka Waziri Mkuu ajiuzulu kutokana na kuongezeka matatizo ya kiuchumi na maandamano ya mara kwa mara ya wananchi.

 

Youssef Chahed, Waziri Mkuu wa Tunisia

Wakosoaji wa Chahed wanasema kuwa serikali yake imeshindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kiuchumi unaoisumbua Tunisia na kwa sababu hiyo wamemtaka Waziri Mkuu na baraza lake la mawaziri wajiuzulu.