Kobler: Uvamizi wa kijeshi dhidi ya Libya ulikuwa makosa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i4909-kobler_uvamizi_wa_kijeshi_dhidi_ya_libya_ulikuwa_makosa
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi nchini humo ulikuwa makosa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 12, 2016 11:29 UTC
  • Kobler: Uvamizi wa kijeshi dhidi ya Libya ulikuwa makosa

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema kuwa uingiliaji kijeshi wa nchi za Magharibi nchini humo ulikuwa makosa.

Martin Kobler amekosa mashambulizi ya kijeshi ya nchi za Magharibi dhidi ya Libya na kusisitiza kuwa, nchi hiyo inahitaji jeshi la taifa ili kuendesha vita dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh.

Kobler ameongeza kuwa nchi za Magharibi mwaka 2011 zilifanya kosa kubwa kwa kuishambulia Libya kwa sababu wakati nchi hizo zilipochukua uamuzi huo zilipasa pia kufikiria marhala na kipindi cha baada ya uvamizi huo.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amekiri kuwa, nchi za Magharibi zinafuatilia malengo yao binafsi huko Libya. Kobler amesema hali ya kibinadamu nchini Libya ni mbaya na kwamba watoto wa nchi hiyo hawapatiwi huduma ya chanjo kutokana na kuendelea kufungwa shule nchini humo.

Martin Kobler ameyasema hayo baada ya Rais Barack Obama wa Marekani kukiri Jumapili iliyopita kuwa kosa kubwa zaidi alilolifanya katika kipindi cha utawala wake ni kuandaa mpango wa kuishambulia Libya.