Mwanasiasa nchini Tunisia: Mohammad Bin Salman hana nafasi ndani ya nchi yetu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i49753-mwanasiasa_nchini_tunisia_mohammad_bin_salman_hana_nafasi_ndani_ya_nchi_yetu
Mwakilishi wa Bunge nchini Tunisia amelalamikia vikali uamuzi wa Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia wa kuitembelea nchi hiyo na kusisitiza kwamba, Bin Salman ambaye ni muuaji mkubwa, hana nafasi ndani ya nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 25, 2018 13:25 UTC
  • Bin Salman
    Bin Salman

Mwakilishi wa Bunge nchini Tunisia amelalamikia vikali uamuzi wa Mohammad Bin Salman, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia wa kuitembelea nchi hiyo na kusisitiza kwamba, Bin Salman ambaye ni muuaji mkubwa, hana nafasi ndani ya nchi hiyo.

Imed Daïmi wa harakati ya Irada nchini Tunisia na mjumbe wa Kamati ya Usalama na Ulinzi katika Bunge la Tunisia ameeleza upinzani wake dhidi ya safari ya mwanamfalme huyo wa utawala wa Aal-Saud na kutoa ujumbe unaosisitiza: 'Muuaji Bin Salman hakaribishwi Tunisia.' 

Imed Daïmi ameashiria pia suala la kuhusika Bin Salman katika kutekwa na kuuawa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari na mkosoaji wa utawala wa Saudia ndani ya ubalozi mdogo wa nchi hiyo mjini Istanbul, Uturuki na kusema: "Yeye binafsi, wabunge wengi na raia wa Tunisia wanapinga vikali safari ya muuaji huyo wa Jamal Khashoggi."

Imed Daïmi, mwakilishi wa bunge nchini Tunisia

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii katika nchi za Kiarabu wamepinga vikali safari hiyo kutokana na jinai zinazofanywa na mrithi huyo wa kiti cha ufalme nchini Saudia, ikiwemo hatua yake ya kuendeleza vita na mauaji nchini Yemen, hujuma na mzingiro wa muungano vamizi unaoongozwa na Saudia dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo, mauaji yake dhidi ya Khashoggi na juhudi zake za kuboresha uhusiano wa Riyadh na utawala katili wa Israel.

Sambamba na kuanza safari ya kwanza ya Bin Salman nje ya nchi tangu baada ya mauaji ya Khashoggi, kumeongezeka mashinikizo kutoka kwa raia wa nchi zinazotembelewa wanaopinga safari ya mwanamfalme huyo wa Saudia. Bin Salman anatembemea nchi za Imarati, Bahrain, Misri, Tunisia, Algeria na Mauritania.