Kufungwa ofisi ya televisheni ya al Jazeera nchini Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53827-kufungwa_ofisi_ya_televisheni_ya_al_jazeera_nchini_sudan
Viongozi wa Sudan wameagiza kusimamishwa shughuli za televisheni ya al Jazeera nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2019 03:27 UTC
  • Kufungwa ofisi ya televisheni ya al Jazeera nchini Sudan

Viongozi wa Sudan wameagiza kusimamishwa shughuli za televisheni ya al Jazeera nchini humo.

Sambamba na kufanyika kikao cha Makka; viongozi wa Sudan wameagiza kufungwa ofisi ya televisheni ya al Jazeera huko Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo na kubatilishwa vibali vyote vya televisheni hiyo. 

Tovuti ya habari ya al Jazeera imethibitisha taarifa ya kufungwa ofisi yake huko Khartoum na kuandika kuwa maafisa usalama wa Sudan wamesema kuwa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan ndilo lililoagiza kuchukuliwa hatua hiyo. Viongozi wa Sudan hata hivyo hawajataja sababu iliyopelekea kufungwa ofisi na kusimamishwa shughuli za televisheni ya al Jazeera nchini humo. Televisheni hiyo imeitaja hatua ya Sudan ya kufunga ofisi yake huko Khartoum kuwa ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa vyombo vya habari. Viongozi wa Sudan wameitaja sehemu walipokusanyika wafanya maandamano karibu na jengo la Wizara ya Ulinzi kuwa ni tishio kwa usalama wa taifa.  

Televisheni ya al Jazeera na maandamano ya wananchi wa Sudan  
 

Televisheni ya al Jazeera imeripoti kuwa msemaji mmoja wa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan ametangaza kupitia televisheni nchini humo kuwa mtu yoyote atakayekaribia jengo la Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo atachukuliwa hatua zipasazo.