Baraza la kijeshi la mpito Sudan: Hakuna wafungwa wa kisiasa nchini humo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54351-baraza_la_kijeshi_la_mpito_sudan_hakuna_wafungwa_wa_kisiasa_nchini_humo
Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan amedai kuwa hakuna mfungwa yoyote wa kisiasa aliyeko hivi sasa katika jela za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 25, 2019 08:25 UTC
  • Baraza la kijeshi la mpito Sudan: Hakuna wafungwa wa kisiasa nchini humo

Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan amedai kuwa hakuna mfungwa yoyote wa kisiasa aliyeko hivi sasa katika jela za nchi hiyo.

Muhammad Hamdan Dagalo amekanusha kuwepo wafungwa wa kisiasa huko Sudan na kupinga kufikiwa makubaliano yoyote na muungano wa wapinzani ikiwemo Harakati ya Uhuru na Mabadiliko kuhusiana na suala la kuundwa baraza la uongozi kabla ya kubuniwa bunge. Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan amezitolea wito pande zote za Sudan kushirikiana ili kufikia mapatano. 

Jenerali Muhammad Haman Dagalo, Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Sudan

Hii ni katika hali ambayo baraza hilo la kijeshi linaloongoza Sudan limepinga mipango iliyopendekezwa na Umoja wa Afrika kwa ajili ya kupunguza mivutano na kuwezesha kufikiwa mapatano kati ya baraza hilo na makundi ya kisiasa. Huku haya yakiripotiwa, maandamano dhidi ya baraza hilo la kijeshi yangali yanaendelea. 

Baraza la kijeshi la mpito linaloongoza Sudan lilishika madaraka ya nchi baada ya kufanya mapinduzi tarehe 11 Aprili mwaka huu na kumng'oa madarakani Rais Omar al Bashir, hata hivyo wananchi wa Sudan wanaendelea kuandamana wakisisitiza  kuundwa serikali ya kiraia nchini humo.