Baraza la Kijeshi Sudan lawaonya wapinzani kuhusu maandamano ya leo Jumapili
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i54448-baraza_la_kijeshi_sudan_lawaonya_wapinzani_kuhusu_maandamano_ya_leo_jumapili
Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan linaloongoza nchi hiyo limeonya kuwa muungano wa wapinzanio na wafanya maandamano watabeba dhima ya hasara au vifo vitakavyotoea kufuatia maandamano waliyopangwa kufanyika leo Jumapili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 29, 2019 23:44 UTC
  • Baraza la Kijeshi Sudan lawaonya wapinzani kuhusu maandamano ya leo Jumapili

Baraza la Kijeshi la Mpito la Sudan linaloongoza nchi hiyo limeonya kuwa muungano wa wapinzanio na wafanya maandamano watabeba dhima ya hasara au vifo vitakavyotoea kufuatia maandamano waliyopangwa kufanyika leo Jumapili.

Itakumbukwa kuwa Muungano wa Harakati ya Uhuru na Mabadiliko (FFC) umetoa wito wa kufanyika maandamano ya watu milioni moja katika mitaa ya mji mkuu wa Sudan, Khartoum kwa lengo la kushinikiza matakwa yake ukilitaka baraza hilo la kijeshi kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.  

Majenerali wa jeshi na muungano wa upinzani nchini Sudan wamekuwa wakipishana kwa wiki kadhaa sasa kuhusu namna ya kusimamia kipindi cha mpito nchini humo kuelekea uchaguzi baada ya jeshi la Sudan kumpindua Rais wa nchi hiyo Omar al Bashir Aprili 11 mwaka huu aliyedumu uongozini kwa muda mrefu.

Omar Hassan al Bashir, Rais wa Sudan aliyepinduliwa na jeshi

Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo Naibu Mkuu wa Baraza la Kijeshi la Uongozi wa Mpito la Sudan ametahadharisha  kuhusu eti njama na ajenda ya ambayo imepangwa na wapinzani kupitia maandamano ya leo Jumapili. 

Juzi Ijumaa baraza la kijeshi la Sudan lilisema kuwa pendekezo la Umoja wa Afrika na Ethiopia lililotolewa Alhamisi iliyopita linafaa kwa ajili ya kuanza mazungumzo na upande wa upinzani.