Bunge la Tunisia lachunguza njama ya mapinduzi nchini humo
Spika wa Bunge la Tunisia ametangaza kuwa kumeundwa kamati ya kuchunguza njama ya kufanya mapinduzi nchini humo kufuatia hali mbaya ya kiafya ya Rais Beji Caid al Sebsi wa nchi hiyo.
Muhammad al Nasir amesema leo katika Bunge la Tunisia kuwa wakuu wa mirengo mbalimbali bungeni wameafiki kuundwa kamati ya bunge ambayo itachunguza njama ya kutaka kufanya mapinduzi. Spika wa Bunge la Tunisia ameongeza kuwa, viongozi wa mirengo kadhaa katika bunge la nchi hiyo wameashiria njama za baadhi ya pande za kutumia vibaya hali ya kiafya ya Rais al Sebsi ili kufanya mapinduzi dhidi ya serikali na ametoa wito wa kufanyika uchunguzi katika uwanja huo.
Hali mbaya ya kimwili na kiafya ya Rais al Sebsi wa Tunisia na kulazwa kwake hospitalini Alhamisi iliyopita vimeibua malumbano ya kisiasa na mjadala mkubwa katika vyombo vya habari nchini humo. Vilevile kumuukuwepo tetesi kwamba baadhi ya pande nchini humo kikiwemo chama cha An Nahdhah zimefanya jaribio la mapinduzi na kuratibu mipango ya kumuuzulu Muhammad al Nasir Spika wa Bunge la nchi hiyo aliye na nafasi yake kuchukuliwa na Abdulfatah Mourou.
Hafidh mwana wa Rais Caid al Sebsi wa Tunisia jana alisema kuwa baba yake ameshatoka katika hospitali ya kijeshi na kwamba hali yake inaridhisha. Amesema kwamba Rais Caid al Sebsi ataanza kazi zake kama kawaidia siku chache zijazo.
Hafidh ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya chama cha An Nahdhah cha Tunisia ameongeza kuwa wanapasa kujifunza na kupata ibra kwa matukio yote yaliyojiri nchini humo siku kadhaa zilizopita.