UNAMID yapongeza mapatano ya amani huko Darfur nchini Sudan
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i58224-unamid_yapongeza_mapatano_ya_amani_huko_darfur_nchini_sudan
Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AU wa kulinda amani Darfur Sudan UNAMID, umepongeza mpango wa makubaliano uliotiwa saini baina ya serikali ya mpito ya Sudan na kundi la wabeba silaha la Darfur linaloitwa Darfur Track.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 31, 2019 09:35 UTC
  • UNAMID yapongeza mapatano ya amani huko Darfur nchini Sudan

Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika AU wa kulinda amani Darfur Sudan UNAMID, umepongeza mpango wa makubaliano uliotiwa saini baina ya serikali ya mpito ya Sudan na kundi la wabeba silaha la Darfur linaloitwa Darfur Track.

Mapatano hayo yalitiwa saini wakati wa mazungumzo ya amani yaliyofanyika Juba Sudan kusini mnamo tarehe 28 Desemba 2019.

Mwakilishi wa Pamoja wa UNAMID Jeremiah Mamabolo, amepongeza utiwaji saini wa mkakati huo wa makubaliano na kusema ni hatua chanya inayothibitisha utashi wa kisiasa na dhamira ya pande zote katika kufikia makubaliano ya kina ya amani. UNAMID imekuwa ikitoa msaada wa kiufundi kwa pande zote za Sudan zinazoshiriki majadiliano ya amani Juba tangu tarehe 10 Desemba 2019. 

Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Sudan Abdalla Hamdok

Azimio hilo la Baraza la Usalama liliipa jukumu UNAMID kutoa msaada muhimu unaohitajika kwa serikali ya mpito ya Sudan na makundi yenye silaha yanayoshiriki majadiliano hayo ili kusogeza mbele mchakato wa amani.

Wakati akiapishwa mwezi Septemba, Waziri Mkuu wa Serikali ya Mpito ya Sudan Abdalla Hamdok alisema kuwa, serikali yake inatoa kipaumbele kwa suala la kuhitimishwa vurugu na machafuko ya ndani nchini humo na kuandaa mazingira mazuri ya kuelekea uchaguzi mkuu ujao.