Bunge la Tunisia limelaani mapatano kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62879-bunge_la_tunisia_limelaani_mapatano_kati_ya_imarati_na_utawala_wa_kizayuni
Bunge la Tunisia limelaani mapatano yaliyofikiwa ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 18, 2020 02:27 UTC
  • Bunge la Tunisia limelaani mapatano kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni

Bunge la Tunisia limelaani mapatano yaliyofikiwa ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) na utawala ghasibu wa Israel.

Bunge la Tunisia jana Jumatatu lilitoa taarifa na kuyataja mapatano hayo kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni kuwa ni ukiukaji wa haki za wananchi wa Palestina na ni tishio la waziwazi na limelaani mapatano hayo. 

Taarifa ya bunge la Tunisia pia imesisitiza kuiunga mkono kadhia ya Palestina kama kipaumbele cha Ulimwengu wa Kiislamu. Bunge la Tunisia na wananchi wa nchi hiyo wamesisitiza juu ya upinzani wao kwa siasa za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na utawala wa Kizayuni.  

Bunge la Tunisia limeutaka muungano wa mabunge ya nchi za Kiarabu na pia kwa mabung ya kieneo na kimataifa  ulaani mapatano hayo kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni na kuchukua msimamo wa wazi katika kuuunga mkono haki za Palestina. 

Imarati na Israel zafikia mapatano ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya pande mbili  

Utawala wa Kizayuni na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) tarehe 13 mwezi huu zilitoa taarifa ya pamoja na kutangaza kuwa: Abu dhabi na Tel Aviv zinahuisha rasmi uhusiano kati yao. Mapatano hayo yamekosolewa pakubwa katika Ulimwengu wa Kiislamu.