Rais wa Tunisia apinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i68672-rais_wa_tunisia_apinga_kufanyiwa_marekebisho_mahakama_ya_katiba
Rais wa Tunisia amemtumia ujumbe Spika wa Bunge la nchi hiyo akipinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 04, 2021 23:58 UTC
  • Rais wa Tunisia apinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba

Rais wa Tunisia amemtumia ujumbe Spika wa Bunge la nchi hiyo akipinga kufanyiwa marekebisho Mahakama ya Katiba ya nchi hiyo.

Katika ujumbe wake huo kwa Spika wa Bunge, Rais Kais Saeid wa Tunisia amesisitiza tena ulazima wa kuheshimiwa sheria na kanuni zote za Katiba na kujiepusha na maoni yote yasiyofaa. 

Bunge la Tunisia tarehe 25 mwezi Machi mwaka huu lilipasisha rasimu ya katiba kwa ajili ya kuifanyia marekebisho na kukamilisha sheria nambari 50 ya mwaka 2015 kuhusu Mahakama ya Katiba. Wabunge 111 wa Bunge la Tunisia wameunga mkono rasimu hiyo huku wabunge watano wakijizuia kupiga kura. Hakuna kura ya hapana iliyopigwa kwa rasimu hiyo. 

Bunge la Tunisia 

Kwa mujibu wa katiba ya Tunisia, Rais wa nchi ana haki na mamlaka ya kuurejesha mswada bungeni kwa kuainisha sababu zilizompelekea kuchukua hatua hiyo ili uweze kuchunguzwa upya.