Maandamano dhidi ya ukandamizaji wa polisi yaendelea huko Tunis, Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i71312-maandamano_dhidi_ya_ukandamizaji_wa_polisi_yaendelea_huko_tunis_tunisia
Maandamano ya usiku ambayo yamekuwa yakifanywa kwa siku kadhaa sasa na wakazi wa mji mji mkuu wa Tunisia, Tunis yameripotiwa kushika kasi. Maandamano hayo yameshuhukiwa katika vitongoji viwili huko Tunis.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 15, 2021 22:39 UTC
  • Maandamano dhidi ya ukandamizaji wa polisi yaendelea huko Tunis, Tunisia

Maandamano ya usiku ambayo yamekuwa yakifanywa kwa siku kadhaa sasa na wakazi wa mji mji mkuu wa Tunisia, Tunis yameripotiwa kushika kasi. Maandamano hayo yameshuhukiwa katika vitongoji viwili huko Tunis.

Makumi ya vijana wa Tunisia wamefanya maandamano katika vitongoji viwili katika wilaya ya Sidi Hassine kulalamikia ukandamizaji na utumiaji mabavu wa polisi ya nchi hiyo na kusababisha kifo cha mkazi wa wilaya hiyo kwa jina la Ahmad bin Ammar ambaye aliaga duna hivi karibuni akiwa katika seli ya polisi. Maandamano hayo yametibuka na kuwa fujo baada ya polisi kuingilia kati. 

Askari usalama wa Tunisia wametumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji. Wakazi wa wilaya ya Sidi Hassine kwa usiku wa sita sasa wanafanya maandamano kufuatia kuaga dunia raia hiyo katika seli ya polisi tarehe 8 mwezi huu wa Juni. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia Alhamisi iliyopita ilikanusha kuwa kifo kijana huyo hakijasababishwa na utumiaji mabavu wa polisi alipotiwa mbaroni. Askari usalama nchini Tunisia tena hawana mamlaka ya juu baada ya kupita miaka 10 tangu kuhitimishwa utawala wa kijeshi wa Zainul Abidin bin Ali, hata hivyo katika kipindi chote hicho hakuna marekebisho makubwa yaliyojiri huko Tunisia bali vitendo vya ukandamizaji na unyanyasaji wa polisi nchini humo vimekuwa vikifuatiliwa kisheria kwa nadra sana.