Waethiopia wapiga kura katika uchaguzi muhimu wa Bunge
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i71514-waethiopia_wapiga_kura_katika_uchaguzi_muhimu_wa_bunge
Mamilioni ya wananchi wa Ethiopia mapema leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kwa ajii ya kuchagua wawakilishi wao katika Bunge la nchi hiyo, uchaguzi ambao umesusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 21, 2021 10:33 UTC
  • Waethiopia wapiga kura katika uchaguzi muhimu wa Bunge

Mamilioni ya wananchi wa Ethiopia mapema leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kwa ajii ya kuchagua wawakilishi wao katika Bunge la nchi hiyo, uchaguzi ambao umesusiwa na baadhi ya vyama vya upinzani.

Waethiopia milioni 37 waliotimiza masharti ya kupiga kura wanachagua wabunge 547 kati ya wagombea wote zaidi ya elfu nane wa vyama 46 vya siasa waliojiandikisha kuwania viti hivyo. Idadi ya waliojisajili kupiga kura imetajwa kuwa ni ndogo ikizingatiwa kuwa Ethiopia ina jamii ya watu milioni 110.

Uchaguzi wa Bunge la Ethiopia haufanyiki kwenye majimbo ya Tigray na Somalia kutokana na hali mbaya ya usalama na machafuko yanayoendelea katika maeneo hayo.

Uchaguzi wa Bunge nchini Ethiopia unafanyika huku nchi hiyo ikisumbuliwa na migogoro ya ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vita katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo la Tigray na mgogoro wa Addis Ababa na nchi za Misri na Sudan juu ya ujenzi wa Bwawa la Renaissance juu ya mali ya Mto Nile.

Abiy Ahmed

Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imeahidi kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki, na kwamba ndio utakaokuwa wa kidemokrasia zaidi katika historia ya Ethiopia.

Ripoti zinasema kuwa chama cha Prosperity kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed kinaongzoa katika majimbo mengi ya uchaguzi.