Tebboune: Algeria si koloni tena la Ufaransa
Rais wa Algeria imetangaza kuwa Ufaransa inapasa kusahau kuwa Algeria ni nchi iliyokoloniwa.
Rais Abdelmajid Tebboune amesema kuwa Ufaransa iliwaua kwa umati na kutekeleza jina chungu nzima dhidi ya Waalegria katika miaka 70 ya vita huko Algeria. Rais wa Algeria ameashiria namna Paris inavyopasa kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa na nchi mbili hizo mwaka 1968 na kuongeza kuwa, matamshi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuidhalilisha Algeria ni matamshi yaliyojaa upotoshaji na yenye chuki kwa lengo la kampeni za uchaguzi.
Rais wa Algeria amesema, balozi wa nchi hiyo atarejea Ufaransa kwa sharti kwamba Paris iiheshimu kikamilifu Algeria. Amesisitiza kuwa Ufaransa inapasa kusahau kuwa Algeria ilikuwa nchi koloni lake.
Serikali ya Algeria hivi karibuni ilimwita nyumbani kwa mashauriano balozi wake mjini Paris kufuatia matamshi ya karibuni dhidi ya Algeria ya Rais Emmanuel Macron. Rais wa Ufaransa aliwahi kudai kuwa historia ya Algeria haitokani na uhakika wa mambo bali matamshi ya chuki dhidi ya Ufaransa. Algeria ilikoloniwa na Ufaransa kwa muda wa miaka 132.
Vita vya kupigania uhuru wa Algeria vilijiri kuanzia mwaka 1954 hadi 1962; na watu zaidi ya milioni moja na laki tano waliuawa kwenye vita hivyo sambamba na kukandamizwa pakubwa wapigania ukombozi na uhuru wa Algeria.