Bunge la Libya lapendekeza uchaguzi wa rais uakhirishwe kwa miezi sita
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i78560-bunge_la_libya_lapendekeza_uchaguzi_wa_rais_uakhirishwe_kwa_miezi_sita
Baraza la Wawakilishi (Bunge) la Libya limependekeza kuwa ucahguzi wa rais nchini humo uakhirishwe kwa miezi sita.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 29, 2021 04:23 UTC
  • Bunge la Libya lapendekeza uchaguzi wa rais uakhirishwe kwa miezi sita

Baraza la Wawakilishi (Bunge) la Libya limependekeza kuwa ucahguzi wa rais nchini humo uakhirishwe kwa miezi sita.

Kikao hicho cha bunge hilo lililoko mjini Tobrouk kimeitishwa kujadili uchaguzi wa rais ulioakhirishwa na ambao ulikuwa umepangwa kufanyika Disemba 24.

Kaimu Spika wa Bunge Fawzi Al Nuwairi amewasilisha mapendekezo kadhaa kwa wabunge iikiwa ni pamoja na kuakhirisha uchaguzi kwa miezi ista.

Wiki iliyopita, Tume ya Uchaguzi Libya ilipendekeza uchaguzi huo ufanyike baada ya mwezi moja kufuatia vizingiti vilivyoibuka katika kutayarisha uchagguzi huo.

Al Nuwairi ametaka tume hiyo itoe maelezo yenye kukinaisha kuhusu sabababu ambazo zimepelekea uchaguzi uakhirishwe.

Tume hiyo ya uchaguzi ya Libya imependekeza uchaguzi wa bunge ufanyike mwezi Februari 2022 baada ya kufanyika maandamano mbele ya jengo la tume hiyo ya watu wanaolalamika kwamba hivi sasa mazingira mazuri hayajaandaliwa ya kufanyika uchaguzi kama huo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehimiza kufanyika uchaguzi mkuu wa Bunge na Rais katika tarehe mwafaka nchini Libya.

António Guterres alitoa mwito huo usiku wa kuamkia Ijumaa na huku akigusia tangazo la tarehe 22 Disemba la Tume Kuu ya Uchaguzi ya Libya la kuakhirisha uchaguzi huo na kutangazwa tarehe mpya ya kufanyika kwake, amesema, uchaguzi wa Rais na Bunge la Libya unapaswa kufanyika katika wakati unaofaa kwa lengo la kuhakikisha makabidhiano ya madaraka yanafanyika kwa amani na kwa njia ya kidemokrasia.