Jun 07, 2016 03:29 UTC
  • Kituo cha Kiislamu Nigeria chagharamia  operesheni ya macho katika mwezi wa Ramadhan

Kituo cha uratibu cha Waislamu nchini Nigeria kimetangaza kujitolea kugharamia operesheni ya macho kwa raia kwa mnasaba wa kuingia mwezi mtukufu wa Ramdhani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo kituo hicho kimetangaza kujitolea kugharamia operesheni 200 za macho katika majimbo mawili ya Lagos na Kaduna nchini humo. Disu Kamor, mkuu wa kituo hicho aliyasema hayo jana Jumatatu na kuongeza kuwa, msaada huo umetolewa kwa mnasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kamor ameongeza kuwa, mwaka 2015 kituo hicho pia kilijitolea kusimamia gharama ya operesheni 240 katika majimbo ya Niger, Kwara na Kogi. Kadhalika amesema kuwa lengo la msaada huo ni kuwasaidia watu wenye matatizo na kusisitiza kuwa, msaada huo unawahusu watu wote na si Waislamu peke yao. Katika sehemu nyingine kituo hicho kimetangaza mpango mpya wa kusambaza maji katika maeneo yanayokabiliwa na uhaba wa maji nchini Nigeria.

Tags