Jun 17, 2016 14:34 UTC
  • Waasi wa Delta: Ni sisi tulishambulia bomba la mafuta la Akwa Ibom

Waasi wa Ulipizaji Kisasi wa Niger Delta nchini Nigeria wametangaza kuhusika na shambulio dhidi ya bomba la mafuta katika jimbo la Akwa Ibom.

Taarifa iliyotolewa na waasi hao kupitia mtandao wa kijami wa Twitter imeelezea kundi hilo kuhusika na hujuma ya bomba hilo la mafuta katika jimbo la Akwa Ibom, kusini mwa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo polisi ya Nigeria ilikuwa imetangaza kuwa, mlipuko wa bomba hilo ulisababishwa na kumwagika mafuta na kwamba haukuhusiana na shambulio la waasi. Waasi wa Niger Delta wamekuwa wakifanya mashambulizi dhidi ya taasisi za mafuta zinazohusiana na shirika la kitaifa la mafuta la nchi hiyo kadhalika shirika la Shell. Kwa mujibu wa waasi hao, utajiri wa kitaifa unaotokana na nishati hiyo muhimu, haugawiwi kwa usawa baina ya Wanigeria wote.

Tags