-
Somalia yazindua mpango wa chanjo nchi nzima ili kukabiliana na surua, polio na nimonia
May 19, 2025 08:21Somalia leo Jumatatu imezindua kampeni ya chanjo ya kitaifa ili kukabiliana na magonjwa ya surua, polio na nimonia. Kampeni hiyo ya chanjo imekusudia kuwafikia watoto zaidi ya milioni 3 nchini humo.
-
Kenya yasema kurudishwa nyumbani Karua hakutaathiri uhusiano na Tanzania
May 19, 2025 08:10Msemaji wa serikali ya Kenya amesema kuwa kuondoshwa kwa Martha Karua nchini Tanzania hakutavuruga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Tanzania.
-
Sisi katika mkutano na afisa wa US, ataka kusitishwa mapigano Gaza
May 19, 2025 03:39Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi jana Jumapili alitoa wito wa kufikiwa makubaliano ya usitishaji vita mara moja katika Ukanda wa Gaza, na kuruhusu kuingia misaada ya kibinadamu katika eneo hilo lililozingirwa.
-
Jeshi la Sudan latwaa tena eneo la kimkakati Darfur Kaskazini kutoka kwa RSF
May 19, 2025 03:36Jeshi la Sudan limefanikiwa kutwaa tena udhibiti wa eneo muhimu la kistratajia la Attrun huko Darfur Kaskazini kutoka kwa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Profesa Janabi ashinda kiti cha Mkurugenzi wa WHO Afrika
May 18, 2025 23:57Profesa Mohammed Janabi kutoka Tanzania ameshinda uchaguzi wa kuwania kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika.
-
Ethiopia yataka matumizi mazuri ya AI kwa ajili ya maendeleo Afrika
May 18, 2025 23:40Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ametoa mwito kwa nchi za Afrika kufanya jitihada za pamoja za kutumia vizuri Akili Mnemba (AI) nyumbani ili kutia nguvu ustawi na maendeleo ya bara hilo.
-
Sekta zilizoathiriwa zaidi na vita vya Sudan ni umeme na uchukuzi
May 18, 2025 23:39Sekta za umeme na uchukuzi nchini Sudan zimekuwa miongoni mwa sekta zilizoathiriwa zaidi na mzozo wa miaka miwili kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Je, tishio jipya kwa amani ya Ethiopia ni nini?
May 18, 2025 23:39Uamuzi wa serikali ya Ethiopia wa kufuta hadhi ya kisheria ya Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) umeibua wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa amani nchini humo.
-
Wanasheria wa Kenya wakiongozwa na Karua wazuiwa kuingia Tanzania
May 18, 2025 08:20Mwanasiasa maarufu wa Kenya Martha Karua ambaye pia ni mwanasheria anayewakilisha vigogo wa upinzani wanaokabiliwa na kesi katika mataifa jirani, amekamatwa nchini Tanzania katika uwanja wa ndege.
-
Waziri Mkuu wa Ethiopia atoa wito kwa Afrika kuendeleza Akili Mnemba ya ndani
May 18, 2025 05:47Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kuunganisha nguvu katika kuendeleza teknolojia ya Akili Mnemba (AI) ya ndani, ili kuchochea utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya bara.