-
Ajali ya basi yaua watu 42 nchini Afrika Kusini
Oct 13, 2025 05:59Watu wasiopungua 42 wamepoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kubingiria katika jimbo la Limpopo, kaskazini mwa Afrika Kusini.
-
Waislamu wa Nigeria washerehekea usitishaji vita Gaza
Oct 13, 2025 02:54Wanachama wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria katika Jimbo la Bauchi wamesherehekea makubaliano ya kusitisha vita Gaza, ambayo yanaruhusu maelfu ya watu kurejea kwenye nyumba zao zilizobomolewa katika ukanda wa Gaza, kuondolewa kwa vikosi vya mauaji ya halaiki ya Israel na kubadilishana mateka.
-
Mabinti barani Afrika watoa wito wa kuheshimiwa haki zao
Oct 13, 2025 02:54Mabinti barani Afrika wametoa mwito wa kuheshimiwa na kupatiwa kipaumbele haki zao za kimsingi. Wito huo umetolewa katika kongamano la kieneo la mabinti magharibi mwa Afrika. Imeelezwa kuwa, haki za mabinti Afrika ni sauti ambayo haiwezi tena kupuuzwa.
-
AU yataka pande hasimu Madagascar kustahamiliana na kufungua mlango wa mazungumzo
Oct 12, 2025 22:58Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC) Mahmoud Ali Youssouf jana Jumapili alizitaka pande zinazozozana nchini Madagascar kujizuia na kuvulimiana ili kufungua mlango wa mazungumzo wa kutatuliwa kisiasa mvutano uliozuka nchini humo.
-
Serikali ya Sudan: Waasi wa RSF wameua raia 57 wengine El Fasher
Oct 12, 2025 22:57Serikali ya Sudan imetangaza kwamba shambulizi la droni na ndege zisizo na rubani za Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF limeua raia 57 katika makazi yao ya muda ya mji wa El Fasher wa magharibi mwa Sudan.
-
Rais wa Madagascar akanusha taarifa kuwa ametoroka nchi
Oct 12, 2025 07:34Rais Andry Rajoelina wa Madagascar amewahakikishia wananchi kwamba yeye na Waziri Mkuu wanadhibiti hali nchini humo.
-
Wanajeshi wa Madagascar waungana na waandamanaji wanaoipinga serikali katika mji mkuu
Oct 12, 2025 01:55Baadhi ya makundi ya wanajeshi wa Madagascar yamekaidi amri na kuungana na maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali, ambao wamekusanyika katika mji mkuu, Antananarivo, huku maandamano ya kupinga utawala wa Rais Andry Rajoelina yakizidi kupamba moto.
-
Uchaguzi wa Cameroon unafanyika leo huku Biya akitarajiwa kushinda muhula wa nane
Oct 11, 2025 22:53Wananchi wa Cameroon waliotimiza masharti ya kupiga kura leo Jumapili (12 Oktoba) wanaelekea katika vituo vya kupigia kura kushiriki katika uchaguzi wa Rais.
-
Umoja wa Mataifa: Watu milioni 25 wanakabiliwa na baa la njaa Sudan
Oct 11, 2025 22:52Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan vimesababisha mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao na karibu milioni 25 kukumbwa na baa kubwa la njaa.
-
UNHCR yahimiza kuchukuliwa hatua kukabiliana na tatizo kubwa la wakimbizi katika eneo la Sahel
Oct 11, 2025 04:42Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) jana Ijumaa lilitoa wito wa kutekelezwa juhudi za kimataifa haraka iwezekanavyo ili kukabiliana na mgogoro unaoongezeka wa wakimbizi katika eneo la Sahel barani Afrika, ambapo takriban watu milioni 4 wamelazimika kuhama makazi yao huko Burkina Faso, Mali, Niger na katika nchi nyingine jirani.