-
Intifadha ya Nne dhidi ya siasa za vita za Trump na Netanyahu
Dec 08, 2017 23:02Nchi za Kiislamu jana Ijumaa baada ya Swala za Ijumaa zilishuhudia maandamano makubwa ya kupinga Marekani na Israel na kuunga mkono Intifadha na mapambano mapya ya ukombozi wa Palestina.
-
Mahojiano ya Salum Bendera na Sheikh Ali Ammar Mwazoa kuhusu uamuzi wa Trump kuhusiana na Quds + SAUTI
Dec 08, 2017 13:45Waislamu na wapenda haki kote ulimwenguni, jumuiya na asasi za kimataifa zimeendelea kupaza sauti kulalamikia na kuulaani uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kuitangaza Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israe.
-
Mahojiano ya Salum Bendera na Ustadh Muhammad Qassim kuhusu uamuzi wa Trump kuhusiana na Quds + SAUTI
Dec 07, 2017 13:21Uamuzi wa rais wa Marekani wa kuutangaza mji mtakatifu wa Quds wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kulaaniwa na hata waitifaki wa karibu wa Marekani katika kila kona ya dunia.
-
Watanzania watakiwa kutojipweteka kuhusu maambukizi ya Ukimwi + Sauti
Dec 01, 2017 14:27Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan amewaasa wananchi kutobweteka na kuridhika na hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI bali wajali afya zao ili kuweza kufikia lengo la tisini tatu iTapofika mwaka 2020 na kuumaliza kabisa ukimwi nchini Tanzania ifikapo mwaka 2030. Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania milioni 1.4 wanaishi na virusi vya UKIMWI. Mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam Tanzania ana taarifa zaidi.
-
Mazungumzo ya Burundi kuanza Jumanne mjini Arusha Tanzania + Sauti
Nov 27, 2017 14:39Mazungumzo ya kusaka amani nchini Burundi yataanza Jumanne wiki hii mjini Arusha Tanzania chini ya upatanishi wa Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamini Mkapa. Hata hivyo kumekuwa na misimamo tafauti huku baadhi wakiunga mkono mazungumzo hayo; na wengine wakisema majadiliano hayo hayana umuhimu. Mwandishi wetu wa Bujumbura Hamida Issa ametutumia ripoti ifuatayo.
-
Bomoabomoa yazikumba ofisi za Tanesco na Wizara ya Maji nchini Tanzania + Sauti
Nov 27, 2017 14:34Zoezi la bomoabomoa katika ofisi za Tanesco na Wizara ya Maji nchini Tanzania zilizopo katika jiji la Dar es Salaam limeanza rasmi ikiwa ni takribani wiki mbili tu zimepita tangu rais John Pombe Magufuli wa nchi hiyo auagize wakala wa barabara nchini humo Tanroads kufanya zoezi hilo. Taarifa zaidi anazo mwandishi wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam
-
Waislamu Mombasa Kenya walalamikia mavazi ya nusu uchi + Sauti
Nov 24, 2017 02:41Waislamu nchini Kenya wamekosoa vikali tabia ya baadhi ya vijana kuvaa mavazi yasiyo ya heshima na kutoa mwito kwa serikali ya Kenya kuiga mfano wa Uganda ambayo inashinikiza mavazi ya heshima hasa katika maeneo ya umma. Seifullah Murtadha na maelezo zaidi
-
Rwanda kupokea maelfu ya wahamiaji waliokwama Libya + Sauti
Nov 24, 2017 02:36Serikali ya Rwanda imesema kuwa iko tayari kupokea wahamiaji zaidi ya 30,000 wa Kiafrika waliokwama nchini Libya na ambao wanapigwa mnada sokoni na kuuzwa kama bidhaa.
-
Mkutano wa Kimataifa wa Wapenzi wa Ahlul-Baiti AS umeanza leo hapa mjini Tehran + SAUTI
Nov 22, 2017 08:42Mkutano wa Kimataifa wa Wapenzi wa Ahlul-Baiti (as) umeanza leo hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na shakhsia, wanazuoni na wanafikra 500 kutoka katika ulimwengu wa Kiislamu.
-
SAUTI, Ripoti ya Human Right Watch kuhusu unyanyaswaji wa Watanzania huko Uarabuni yazuiliwa na serikali TZ
Nov 14, 2017 15:12Shirika la Kutetea Haki za Binaadamu la Human Right Watch, limezuiliwa kutoa ripoti yake kuhusiana na uchunguzi wa hali ya watumishi wa ndani wa Kitanzania katika nchi za Kiarabu hususan Oman, Umoja wa Falme za Kiarabu na Saudia.