-
SAUTI, Hatimaye waasi wa Ninja wawaachilia huru abiria wa mabasi mawili waliyoyateka, huku wakiwanyang'anya mavazi yao
May 29, 2017 10:45Hatimaye Waasi wa Ninja nchini Congo Brazzaville wamewaachilia huru raia waliowateka nyaraka siku chache zilizopita baada ya juhudi za jeshi la nchi hiyo za kuwaokoa kuambulia patupu.
-
Kiongozi wa Mayazidi Iraq, awataka vijana wa kabila hilo kujiunga na Hashdu Sha'abi
May 29, 2017 09:39Kiongozi Mkuu wa watu wa kabila la Mayazidi nchini Iraq, sambamba na kutoa pongezi na shukurani za dhati kwa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi nchini, amewataka pia vijana wa kabila hilo kujiunga na harakati hiyo kuilinda nchi.
-
Bahram Qassemi: Mapambano dhidi ya uvamizi wa Israel yataendelea
May 29, 2017 09:12Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza juu ya kuendelezwa muqawama na mapambano dhidi ya uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel.
-
Kuongezeka hukumu za kifo dhidi ya wapinzani nchini Saudi Arabia
May 27, 2017 23:13Mahakama kuu ya utawala wa Aal Saud nchini Saudi Arabia imewahukumu adhabu ya kifo wanaharakati 14 kwa kushiriki katika maandamano kwenye eneo la Waislamu wa Kishia la Qatif mwaka 2011.
-
SAUTI: Waasi wa Ninja nchini Congo-Brazzaville wazidi kuwa tishio, waua askari wengi na kuteka mabasi ya abiria
May 27, 2017 10:48Kitendo cha Waasi wa Ninja nchini Congo Brazzaville kuteka mabasi mawili ya abiria katika misitu ya nchi hiyo, kimelifanya jeshi kupatwa na wasi wasi na kutuma helikopta za kijeshi kwa lengo la kuwaokoa watu hao.
-
Ayatullah Khatami: Bahrain imegeuzwa kuwa jela kubwa ya wananchi
May 26, 2017 09:31Khatibu wa Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran sambamba na kulaani hujuma na uvamizi wa vikosi vya usalama vya Bahrain dhidi ya nyumba ya Sheikh Issa Qassim mwanazuoni mashuhuri wa nchi hiyo ametangaza kuwa, utawala wa Aal khalifa kwa kufanya ukandamizaji, kamatakamata na aina mbalimbali za jinai, umeigeuza nchi hiyo na kuwa jela kubwa kwa ajili ya wananchi.
-
SAUTI: Waislamu Kenya: Serikali ya Jubilee isitumie suala la uhuru wa Ramadhani katika kampeni, ni haki ya kila Mkenya
May 23, 2017 13:32Shakhsia mbalimbali wa Kiislamu nchini Kenya, wameitaka serikali kuwahakikishia Waislamu usalama wa kutosha ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya serikali hiyo kuondoa hali ya hatari katika maeneo ya mpakani na Somalia.
-
SAUTI: Polisi ya Kinshasa yawabembeleza wakazi wa mji huo kuwataja wafungwa waliotoroka jela kuu, nao uvamizi wa jela wakikithiri
May 19, 2017 13:41Polisi ya mji wa Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewataka wakazi wa mji huo kuisaidia serikali katika kuwataja wafungwa waliotoka jela kuu ya jiji hilo.
-
SAUTI: Viongozi wa chama cha UDPS Kongo DR wawekwa kizuizini na polisi siku tatu, kuwazuia kujadili kuurejesha mwili wa Tshisekedi
May 13, 2017 14:07Huku mgogoro juu ya suala la kusafirishwa, kuagawa na kuzikwa kwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi kiongozi wa upinzani wa chama cha The Union for Democracy and Social Progress huko Kongo DR, ukiendelea kutokota, jeshi la polisi limewaweka kizuizini kwa siku tatu viongozi wa chama hicho.
-
SAUTI: Kadhia ya kusafirishwa, kuagwa na hatimaye kuzikwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi wa Kongo DR, bado kitendawili
May 12, 2017 12:36Suala la kusafirishwa, kuagwa na hatimaye kuzikwa mwili wa mzee Étienne Tshisekedi kiongozi wa upinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, limeendelea kuwa kitendawili baada ya upande wa serikali na upinzani kushindwa kuafikiana kuhusiana na suala hilo.