"Operesheni ya al-Aqsa imegeuza ndoto ya kuporomoka Israel kuwa uhalisia"
Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ndoto na jinamizi la kuangamia na kupomoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel sasa imegeuka kuwa hali halisi kutokana na Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.
Meja Jenerali Mohammad Baqeri alisema hayo jana Jumapili hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, "Operesheni hii imedhirisha wazi kuwa, hatua za kutapatapa kama kuanzisha uhusiano wa kawaida na Wazayuni, kamwe haziwezi kuzuia kusambaratika kwa utandu wa buibui (israel)."
Shirika la habari la IRNA limenukuu Jenerali Baqeri akisema kuwa, Operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa imefungua ukurasa mpya katika uga wa muqawama na operesheni za wanajihadi wa Kipalestina dhidi ya Wazayuni maghasibu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Jenerali Baqeri ameeleza bayana kuwa, uwezo wa mhimili wa muqawama katika kuunda silaha upo katika hali bora hivi sasa, kwamba hii leo mhimili huo umejitosheleza na haulazimika kuitegemea Iran.
Vikosi vya Brigedi ya Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapmabano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, vimeendelea kufanya mashambulizi makubwa ya roketi na ya nchi kavu dhidi ya Israel.
Operesheni hiyo kubwa na tata ya Muqawama wa Palestina, ambayo ilifanyika kwa kutumia njia za chini ya ardhi, nchi kavu, baharini na angani, pamoja na kurusha maelfu ya maroketi na makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, hadi sasa imepelekea kuangamizwa mamia ya Wazayuni na kujeruhiwa maelfu ya wengine.