Mar 29, 2024 08:01 UTC
  • Spika Qalibaf: Ulimwengu wote wa Kiislamu una wajibu wa kuunga mkono Muqawama wa taifa la Palestina

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amepongeza istikama na kusimama imara kusio na mfano kwa Muqawama na wananchi wa Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel na akasema, Ulimwengu mzima wa Kiislamu una wajibu wa kuliunga mkono taifa la Palestina katika vita visivyo na mlingano na utawala huo wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa IRNA, Mohammad Baqer Qalibaf, jana Alkhamisi alikutana na kufanya mazungumzo na Ismail Haniya, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS na kueleza kuwa operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni hatua ya mabadiliko ya kipekee katika historia ya kisiasa na mapambano ya nchi za Kiislamu na akaongeza kuwa, inapasa Muqawama uelekeze juhudi zake katika nyuga tofauti na wote wanaohusika katika kambi ya Muqawama na mapambano wanapaswa kuchukua hatua za pamoja kupambana na utawala wa Israel mwangamizaji wa kizazi.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Hamas ametoa shukurani kwa mapokezi mazuri waliyopata na kueleza hisia kubwa za mapenzi zilizoonyeshwa na viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono Muqawama wa Palestina na akasema, vita vya hivi sasa ni nukta ya mabadiliko ya kipekee katika historia ya kupambana na utawala wa Kizayuni, na vimekuwa na matokeo makubwa ya kistratejia kwa Palestina, Ulimwengu wa Kiislamu, Ulimwengu wa Kiarabu na ulimwengu mzima; na kwa hivyo ni hakika kwamba, kipindi baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ni tofauti na kipindi cha kabla yake.

Jana hiyohiyo, Spika Qalibaf alifanya mazungumzo pia na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina Ziyad al-Nakhla pamoja na ujumbe aliofuatana nao na kusisitiza kuwa, kwa kuzingatia imani yake na kwa kufuata miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu kamili suala la kuunga mkono kambi ya Muqawama na Palestina.

 
Spika wa Bunge la Iran amesema, ushindi wa hivi karibuni wa Muqawama ni matunda ya istikama na kusimama imara wapiganaji na wananchi wa Palestina na akaongeza kuwa, hii leo baada ya wiki 25 mfululizo za vita vigumu na visivyo na mlingano, inapasa kuwaenzi Mashahidi wa Ghaza na Mashahidi wa miaka ya nyuma waliopelekea kupatikana uwezo uliofikiwa hivi sasa wa kukabiliana na utawala ghasibu wa Kizayuni.
 
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesisitiza kuwa, Muqawama na mapambano ndio njia pekee ya kukabiliana na utawala ghasibu wa Israel.  Al-Nakhla amebainisha kuwa, wananchi wa Palestina wanasimama imara kukabiliana na unyama na ukatili wa utawala wa Kizayuni, Ziyad Al-Nakhlah akaeleza bayana kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeuunga mkono Muqawama wa Palestina kwa uwezo wake wote.../

 

Tags