Jun 27, 2024 12:16 UTC
  • Zakani ajiondoa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa Iran

Alireza Zakani, mgombea wa kiti cha urais kwa muhula wa 14, leo Alhamisi, tarehe 7 Julai, ametoa tamko akitangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwania kiti hicho.

Zakani ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X kwamba amesalia kwenye mashindano hadi mwisho wa wakati wa kisheria wa kampeni za uchaguzi, lakini mwishowe akaamua kwamba kuendelea kwa njia ya Shahid Ebrahim Raisi ni muhimu zaidi. Amewaomba wagombea wengine Jalili na Qalibaf waungane na kuitikia wito halali ya waungaji mkono wa Mapinduzi ya Kiislamu wa kuzuia kuundwa kwa serikali ya watu anaohisi kuwa wanaegemea upande wa kuwa na uhusiano mkubwa na nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikifanya njama dhidi ya Mfumo wa Kiislamu. Amewashukuru wananchi wa Iran kwa kumuunga mkono katika juhudi zake za kuwania kiti cha rais.

Mapema leo asubuhi Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, mgombea mwingine kati ya wagombea sita wa kiti cha rais ajaye wa Iran, alitangaza kujiondoa katika kinyang'anyiro hicho. Uchaguzi huu wa kabla ya wakati wake umepangwa kufanyika kesho Ijumaa tarehe 28 Juni, 2024.