Jun 28, 2024 03:19 UTC
  • Iran yalaani jaribio la mapinduzi lililofeli Bolivia

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani jaribio la mapinduzi lililofeli nchini Bolivia.

Shirika la habaril la IRNA limemnukuu Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran akisema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inakosoa vikali mapinduzi hayo dhidi ya misingi ya demokrasia.

Aidha amesema Iran inalaani na kupinga uvamizi dhidi ya taasisi za kidemokrasia nchini Bolovia, na hujuma dhidi ya serikali halali ya nchi hiyo.

Vyombo vya habari nchini Bolivia vimefichua nafasi ya serikali ya Marekani katika kujiri jaribio hilo la mapinduzi lililotibuliwa nchini humo. Rais Luis Arce amewashukuru wananchi wa Bolivia kwa kuzima mapinduzi hayo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Marekani kuhusishwa na mapinduzi nchini Bolivia. Novemba mwaka 2019, mapinduzi mengine yalifanywa nchini humo kwa usimamizi na ufadhili wa serikali ya Washington.

Jeneral Juan Jose aliyeongeza mapinduzi yaliyofeli akamatwa

Evo Morales ambaye aliibuka na ushindi katika uchaguzi wa rais wa Oktoba mwaka 2019, hatimaye alilazimika kujiuzulu kufuatia kushtadi maandamano ya mitaani yaliyochochewa na Marekani na waitifaki wake; na kukimbilia nchini Mexico. Makumi ya watu waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika machafuko hayo ya kisiasa huko Bolivia 2019.

Marekani imekuwa ikiyumbisha usalama na uthabiti nchini Bolivia kutokana na taifa hilo la Amerika ya Latina kupinga sera za ubeberu za Marekani na kuliunga mkono taifa madhulumu la Palestina. 

Hivi karibuni, Wizara ya Mambo ya Nje ya Bolivia ililaani mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ukanda wa Gaza, na kutoa wito wa kufunguliwa mashtaka Waziri Mkuu wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ). 

Tags