Rais mpya wa Iran: Sera za Iran katika kuitetea Palestina haziwezi kubadilika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i114634-rais_mpya_wa_iran_sera_za_iran_katika_kuitetea_palestina_haziwezi_kubadilika
Rais mpya wa Iran amesema alipoonana na kuzunguzma na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina kuwa misimamo na sera za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwaunga mkono waliodhulumiwa wakiwemo wananchi wa Palestina haziwezi kubadilika.
(last modified 2024-07-30T04:07:18+00:00 )
Jul 30, 2024 04:07 UTC
  • Rais mpya wa Iran: Sera za Iran katika kuitetea Palestina haziwezi kubadilika

Rais mpya wa Iran amesema alipoonana na kuzunguzma na Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina kuwa misimamo na sera za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwaunga mkono waliodhulumiwa wakiwemo wananchi wa Palestina haziwezi kubadilika.

Masoud Pezeshkian jana alikuwa na mazungumzo na Ziyad al Nakhlah Katibu Mkuu wa Jihadul Islami ya Palestina ambapo alieleza kuwa misimamo na sera za mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwaunga mkono waliodhulumika wakiwemo wananchi wa Palestina na malengo yao ya kuikomboa Quds haziwezi kubadilika kwa kuingia madarakani serikali mbalimbali. 

Pezeshkian ameeleza kuwa kuunga mkono na kutetea malengo ya wananchi madhulumu wa Palestina kutaendeleaa kwa nguvu zote na kuwa hakuna jambo litakalokwamisha irada ya Iran katika njia hii. 

Pezeshkian ameongeza kuwa, mazungumzo aliyofanya na Katibu Mkuu wa Jihadul Islami ya Palestina ni ujumbe muhimu kwa wale wote wanaotaka kuibua mwanya kati ya Iran na makundi ya muqawama khususan ndugu na mujahidina wa Kipalestina. 

Wanamuqawama wa Palestina 

Ziyad al Nakhlah Katibu Mkuu wa Jihadul Islami ya Palestina pia ambaye yupo hapa Tehran kwa lengo la kushiriki katika hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran amesema kuwa Wapalestina madhulumu wakazi wa Ukanda wa Gaza hii leo wako mstari wa mbee mkabala wa wapenda makuu na wawakilishi wao katika eneo; na msimamo na sauti madhubuti ya Iran katika kuunga mkono muqawama vina taathira muhimu katika kudumisha ari ya mapambano na istiqama.