Uwezo wa mashambulizi wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran hauwezi kuzuiliwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137398-uwezo_wa_mashambulizi_wa_vikosi_vya_ulinzi_vya_iran_hauwezi_kuzuiliwa
Msemaji wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ya Khatam al‑Anbiya (s) amesema: uwezo wa mashambulizi wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatokana na elimu na teknolojia ya ndani ya nchi; hauwezi kumalizika wala kudhibitiwa kwa namna yoyote.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Mar 16, 2026 05:45 UTC
  • Uwezo wa mashambulizi wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran hauwezi kuzuiliwa

Msemaji wa Kamandi ya Majeshi ya Iran ya Khatam al‑Anbiya (s) amesema: uwezo wa mashambulizi wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatokana na elimu na teknolojia ya ndani ya nchi; hauwezi kumalizika wala kudhibitiwa kwa namna yoyote.

Sehemu ya taarifa kamili ya msemaji huyo iliyochapiswa na Shirika la Habari la IRIB ni kama ifuatavyo:

Adui mhalifu katika maneno yake ya propaganda alidai kuwa uwezo wa mashambulizi wa Iran umeangamizwa. Hata hivyo, katika mawimbi ya operesheni zetu za mashambulizi, tumekuwa tukitekeleza pigo la kipekee na kali, tukitumia mbinu za kivita zisizo za kawaida pamoja na silaha maalumu na za kisasa, kwa mtiririko endelevu na kwa mashambulizi yanayofuatana.

Mawimbi ya hamsini na moja hadi hamsini na nne ya Operesheni Ahadi ya Kweli 4, huku yakidumisha na kuongeza kwa kasi kiwango cha mashambulizi na kupata udhibiti kamili wa anga, yametekelezwa kwa kaulimbiu zenye baraka kama vile “Ewe Ali bin Musa al‑Ridha (a.s.)”, “Ewe Zaynab al‑Kubra (a.s.)”, “Ewe Jawad al‑A’imma, na “Ewe Zahra (a.s.)”.

Katika mawimbi haya makali na yenye athari kubwa, hatua ya kwanza ilihusisha mashambulizi ya pamoja ya makombora dhidi ya vikosi vya jeshi la Marekani la kigaidi katika kambi ya Al‑Kharj. Kituo hiki kinajulikana kama mahali pa kuandaa na kupeleka ndege za kivita za F‑35 na F‑16 za utawala huo wa Marekani, pia ni mahali pa kuhifadhi ndege za kujaza mafuta angani pamoja na kituo kikuu cha ndege za upelelezi za AWACS za Marekani, na kimekuwa chanzo cha mashambulizi dhidi ya nchi yetu. Lengo hilo lilipigwa kwa usahihi.

Baada ya hapo, katika hatua ya kwanza ya kulipiza kisasi kwa damu ya wafanyakazi wanyonge waliouawa shahidi katika miji ya viwanda ya Iran, maeneo kadhaa katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu na vilevile kambi tatu za Marekani katika eneo zilishambuliwa kwa operesheni ya pamoja ya Vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kuharibiwa kwa nguvu kubwa.

Sehemu za viwanda pamoja na maeneo ya mkusanyiko wa wanajeshi wa Marekani katika vituo vitatu vya majeshi ya anga ambavyo ni Al‑Harir Erbil , Ali al‑Salem na Arifjan  pia viliharibiwa kwa makombora na ndege zisizo na rubani za Iran.

Katika mwendelezo wa mashambulizi haya, saa chache zilizopita, operesheni nyingine ilitekelezwa kwa mashambulizi ya pamoja ya makombora na ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga dhidi ya vikosi vya jeshi la Marekani katika kambi ya Al‑Dhafra.

Kambi hii ina jukumu la msaada wa kijasusi na kiutendaji katika mashambulizi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na katika vituo vya uongozi na udhibiti wa kikanda.

Aidha, operesheni nyingine iliyofanikiwa ilitekelezwa kwa kutumia makombora mazito sana aina ya Khorramshahr yenye kichwa cha vita chenye uzito wa tani mbili, pamoja na makombora Kheibar‑Shekan, Qadr, Emad, na kwa mara ya kwanza katika Operesheni Ahadi ya Kweli 4, kombora la kimkakati la Sejjil limetumika. Mashambulizi hayo yalielekezwa dhidi ya vituo vya usimamizi na maamuzi vinavyoongoza operesheni za anga za utawala wa Kizayuni, miundombinu muhimu ya sekta ya kijeshi na ulinzi, pamoja na maeneo ya mkusanyiko wa wanajeshi wa utawala huo, na yalitekelezwa kwa mafanikio.

Tangu alfajiri ya siku ya Jumapili, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani, wanajeshi jasiri wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran walivamia vituo vya usalama na makao ya polisi ya utawala wa Kizayuni, ikiwemo kitengo maalumu cha polisi pamoja na kituo cha mawasiliano ya satelaiti cha utawala huo unaoua watoto.

Uwezo wa mashambulizi wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatokana na elimu na teknolojia ya ndani ya nchi; hauwezi kumalizika wala kuzuiwa.

Msingi wa simulizi ya nguvu huonekana katika uwanja wa mapambano. Idadi ya waliouawa kwa upande wa adui imefikia kiwango ambacho milio ya ambulensi isiyokoma pamoja na kukiri kwa taasisi za Kizayuni imeanza kutikisa sera yao ya kuficha taarifa na ukimya wa makusudi.

“Na ushindi hautoki isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mwenye hekima.”