Msemaji wa IRGC: Uzalishaji wa makombora unaendelea hata wakati wa vita
-
Brigedia Jenerali Ali Mohammad Naeini
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema: "Hakuna wasiwasi katika uwanja wa makombora kwa sababu tunazalisha makombora hata wakati wa vita, jambo ambalo linashangaza, na hakuna tatizo maalumu katika suala la hifadhi ya makombora yetu."
Brigedia Jenerali Ali Mohammad Naeini, msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, amewapongeza wananchi wa Iran kwa kuendelea kuwepo katika medani na nyanjani katika miji na maeneo mbalimbali hapa nchini na kusema: "Kama kungekuwa na alama zaidi ya 120, zinapaswa kutolewa kwa watu hawa."
Ameongeza kuwa: "Matarajio ya wananchi ni kuendelezwa vita hadi adui atakaposhindwa kikamilifu. Vita hivi vitaisha pale kivuli cha vita kitakapoondolewa juu ya nchi yetu."
Akijibu swali kuhusu tasnia ya makombora kwa sasa, msemaji wa IRGC amesema: "Alama ya tasnia yetu ya makombora ni 20 kwa 20 na hakuna wasiwasi katika suala hili, kwa sababu tunazalisha makombora hata wakati wa vita, jambo ambalo linashangaza, na hakuna tatizo maalumu kuhusiana na akiba ya makombora."
Brigedia Jenerali Ali Mohammad Naeini amesema: "Hakika tunayo mambo ya kumshangaza adui. Kadiri tunavyosonga mbele, ndivyo tutakavyokuwa na vita vya kushangaza zaidi, tata, na vilivyojaa mambo ya kustaajabisha."